Al-Baqara
Wannan fassarar tafsirin as-Saʿdī ce, kamar yadda IslamHouse.com ke wallafa ta a saadi.islamenc.com, an karanta ta daga shafukan wannan shafin yanar gizo. Shafin bai faɗi wanda ya fassara ta ba, ko wane bugu da aka buga take bi, kuma bai bayyana sharuɗɗa na ɗaukar rubutunta ba, saboda haka ba a tabbatar da haƙƙin nuna ta ba. Babu wanda ya kwatanta ta da littafin da aka buga, kuma babu malami da ya duba ta. Kowane sashe yana kusa da ayoyin da yake bayani a kansu, waɗanda rubutun Alƙur’ani ne na Tanzil, kamar yadda yake a can; aya da shafin bai ba ta bayani na kanta ba tana tare da sashen da ya gabace ta, kuma jerin yana ambaton kowace irin wannan aya. Sabīl bai rubuta wani abu daga cikinta ba, kuma bai fassara ta ba.
Rubutu dagasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)an ɗauka 2026-10-22
وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِۦ مِنْ خِطْبَةِ ٱلنِّسَآءِ أَوْ أَكْنَنتُمْ فِىٓ أَنفُسِكُمْ ۚ عَلِمَ ٱللَّهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَـٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّآ أَن تَقُولُوا۟ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ۚ وَلَا تَعْزِمُوا۟ عُقْدَةَ ٱلنِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبْلُغَ ٱلْكِتَـٰبُ أَجَلَهُۥ ۚ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِىٓ أَنفُسِكُمْ فَٱحْذَرُوهُ ۚ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ 235
{235} Hii ni hukumu ya mwanamke ambaye anakaa eda ya kufiwa mume. Au yule aliyeachana naye katika uhai kuachana ambako hawawezi kurudiana isipokuwa kwa nikaha mpya. Kwa hivyo, ni haramu kwa asiyekuwa aliyemwacha kumposa waziwazi. Na ndilo lililokusudiwa katika kauli yake, "lakini msiwaahidi kwa siri." Na ama kwa nanma ya kuficha, basi Mwenyezi Mungu amedondoa ubaya ndani yake. Na tafauti baina yake ni kuwa namna ya waziwazi haimaanishi chochote isipokuwa ndoa. Ndio maana ikaharamishwa kwa kuhofia (mwanamke) asije akaharakisha na akadanganya kuhusu kumalizika kwa eda yake kwa sababu ya kutaka kuoleka. Na ndani yake kuna dalili juu ya kuzuia njia za kufikia haramu, na kutimiza haki ya mume wake wa kwanza kwa kutoahidiana na asiyekuwa yeye katika muda wa eda yake. Na ama kwa namna ya kuficha, nayo ni (ile namna) yenye uwezekano wa ndoa na mengineyo. Basi hiyo (namna) inaruhusika kwa yule aliyeachana kuachana kunakolazimu nikaha mpya ili kurudiana, kama vile aseme [amwambie mke huyo]: 'Mimi kwa hakika ninataka kuoa' na 'mimi kwa hakika ningependa unishauri wakati eda yako inaisha,' na mfano wa hayo. Basi hili linaruhusika kwa sababu siyo kama kusema waziwazi. Na ni jambo ambalo huwa kuna msukumo mkubwa wa kulifanya katika nafsi. Na ndio maana alisema, "au mkalificha ndani ya nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu alikwisha jua kwamba nyinyi mtawakumbuka." Na haya maelezo yote ni kuhusiana na utangulizi wa mkataba wa nikaha. Na ama mkataba wa ndoa, huo hauruhusiki, "mpaka andiko (la amri ya eda) lifike muda wake," yani mpaka eda imalizike. "Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu kwa hakika anajua yaliyomo katika nafsi zenu." Yani kusudieni mema, wala msikusudie maovu; kwa kuhofia adhabu yake na kutarajia malipo yake mazuri. "Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe;" kwa anayefanya dhambi kisha akazitubia. Na akarejea kwa Mola wake Mlezi "Mpole" kwa kuwa hakuwaharakishia adhabu waasi juu ya dhambi zao, pamoja na uwezo wake juu yao.