Al-Baqara
Wannan fassarar tafsirin as-Saʿdī ce, kamar yadda IslamHouse.com ke wallafa ta a saadi.islamenc.com, an karanta ta daga shafukan wannan shafin yanar gizo. Shafin bai faɗi wanda ya fassara ta ba, ko wane bugu da aka buga take bi, kuma bai bayyana sharuɗɗa na ɗaukar rubutunta ba, saboda haka ba a tabbatar da haƙƙin nuna ta ba. Babu wanda ya kwatanta ta da littafin da aka buga, kuma babu malami da ya duba ta. Kowane sashe yana kusa da ayoyin da yake bayani a kansu, waɗanda rubutun Alƙur’ani ne na Tanzil, kamar yadda yake a can; aya da shafin bai ba ta bayani na kanta ba tana tare da sashen da ya gabace ta, kuma jerin yana ambaton kowace irin wannan aya. Sabīl bai rubuta wani abu daga cikinta ba, kuma bai fassara ta ba.
Rubutu dagasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)an ɗauka 2026-10-22
كُتِبَ عَلَيْكُمُ ٱلْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰٓ أَن تَكْرَهُوا۟ شَيْـًٔا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰٓ أَن تُحِبُّوا۟ شَيْـًٔا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ 216
{216} Aya hii ina kuwajibishwa kwa kupigana vita katika njia ya Mwenyezi Mungu baada ya kwamba Waumini walikuwa wameamrishwa kuviacha, kwa sababu ya udhaifu wao na kutoweza kwao kustahimili hilo. Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alipohamia Madina, na Waislamu wakawa wengi, wakapata nguvu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaamrisha kupigana vita. Na akajulisha kwamba hilo linachukiza nafsi. Kwa sababu ya uchovu na dhiki vilivyomo ndani yake na kutokea kwa aina mbalimbali za hofu na kujiweka mbele ya mambo yenye kuharibu. Pamoja na hayo, ni nzuri tupu, kwa sababu ya yale yaliyomo ndani yake kama vile thawabu kubwa, kujiepusha na adhabu chungu, kuwashinda maadui, kupata ngawira. Na mengineyo ambayo yanapendwa, pamoja na yaliyomo ndani yake yenye kuchukiza. “Na huenda mkapenda kitu, nacho ni shari kwenu.” Na hilo mfano kutoenda katika vita kwa sababu ya kutafuta starehe. Hilo ni shari (uovu), kwa sababu linasababisha kuachwa na Mwenyezi Mungu. Na kuwapa nguvu maadui juu ya Uislamu na watu wake, kutokea kwa udhalilifu na unyonge, na kupotea kwa malipo makubwa, na kupata adhabu. Aya hizi ni za jumla na zenye kuingia katika kila kitu kwamba matendo mema ambayo nafsi zinazichukia kwa sababu ya ugumu uliomo ndani yake ni heri bila shaka, na kwamba matendo maovu ambayo nafsi zinapenda kwa sababu ya starehe na ladha ambazo zinafikiria kwamba ziko ndani yake, basi hayo ni shari (maovu) bila shaka. Ama hali za dunia, basi hili jambo haliingii katika kila kitu kwa ujumla. Lakini ni aghalabu kwa mja Muumini kuwa akipenda kitu miongoni mwa vitu, kisha Mwenyezi Mungu atamwekea sababu zinazomtolea kitu hicho. Basi hilo ni kheri kwake, na lililo bora kwake katika hayo ni kwamba amshukuru Mwenyezi Mungu, na aweke heri katika hilo lililotokea. Kwa sababu, anajua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye rehema zaidi juu ya waja wake kuliko yeye mwenyewe. Na mwenye uwezo zaidi juu ya masilahi ya mja wake kuliko yeye mwenyewe, na mwenye elimu zaidi juu ya masilahi yake kuliko yeye mwenyewe, kama alivyosema [Mwenyezi Mungu Mtukufu]. “Na Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.” Basi linalofaa zaidi kwenu kwenda pamoja na majaaliwa yake, sawa yatawapendeza au yawawiye mabaya.