Al-An'aam
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ ۖ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَـٰلِقُ كُلِّ شَىْءٍ فَٱعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ وَكِيلٌ 102
{102} Huyo ambaye aliumba alichokiumba, na akakadiria aliyoyakadiria ndiye "Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi;" yaani, mwenye kufanyiwa Uungu, mwenye kuabudiwa, ambaye anastahiki kufanyiwa udhalilifu wa mwisho na mapenzi ya mwisho. Mola Mlezi ambaye alivilea viumbe vyote kwa neema na akaviepushia kila aina ya adhabu, Muumba wa kila kitu, hapana mungu ila Yeye. "Basi muabuduni Yeye," yaani, itakaposimama imara na kuthubiti kuwa Yeye ndiye Mungu, ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye; basi mfayieni aina zote za ibada, na mfanyieni ikhlasi katika hilo, na ukusudieni uso wake katika hayo. Kwa maana Haya ndiyo makusudio ya kuumbwa ambako waliumbwa wa ajili yake. "Sikuwaumba majini na watu isipokuwa waniabudu Mimi tu." "Na Yeye ni Msimamizi wa kila kitu;" maana yake, vitu vyote viko chini ya usimamizi wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji, na uendeshaji, na usimamizi. Na inavyojulikana ni kuwa jambo linaloendeshwa unakuwa unyoofu wake, na utimilifu wake, na ukamilifu wa mpangilio wake kulingana na hali ya mwenye kulisimamia. Na usimamizi wake yeye Mtukufu juu ya mambo si wa aina ya usimamizi wa viumbe. Kwa maana, usimamizi wao ni usimamizi wa uwakilishi, na wakili katika hayo yuko chini ya yule anayemwakilisha. Ama Uwakili wake Yeye Muumba mwanzilishi, mwingi wa baraka, Mtukufu ni uwakili wake kutoka kwake mwenyewe, unaojumuisha ukamilifu wa elimu, na usimamizi mzuri, na kuufanya kwa uzuri zaidi, na uadilifu. Na haiwezekani kwa yeyote yule kumdiriki Mwenyezi Mungu alichokifanya, wala kuona dosari au kasoro katika uumbaji wake, wala upungufu au dosari katika uendeshaji wake mambo. Na katika usimamizi wake ni kuwa Yeye, Mwenyezi, Alijiwekea usimamizi katika kubainisha dini yake na kuihifadhi kutokana na mambo ya kuiondosha na kuibadilisha. Na kwamba yeye Mtukufu alisimamia Kuwahifadhi Waumini na kuwalinda kutokana na yale yanayowaondolea imani na dini yao.