Aller au contenu
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Ankaboot
Sourate 29

Al-Ankaboot

Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.

Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22

Versets 56–59

يَـٰعِبَادِىَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّ أَرْضِى وَٰسِعَةٌ فَإِيَّـٰىَ فَٱعْبُدُونِ 56 كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ ٱلْمَوْتِ ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا تُرْجَعُونَ 57 وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَنُبَوِّئَنَّهُم مِّنَ ٱلْجَنَّةِ غُرَفًا تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۚ نِعْمَ أَجْرُ ٱلْعَـٰمِلِينَ 58 ٱلَّذِينَ صَبَرُوا۟ وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ 59

{56-59} Yeye Mtukufu anasema, "Enyi waja wangu mlioniamini" mimi na mkawasadiki Mitume wangu, "kwa hakika ardhi yangu ina wasaa. Basi niabuduni Mimi peke yangu." Na hamwezi kumwabudu Mola wenu Mlezi katika nchi moja, basi ondokeni huko na muende katika nchi nyingine; ambapo wanamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake; kwa maana maeneo ya ibada na sehemu zake ni pana, na Yule anayeabudiwa ni Mmoja tu, na mauti lazima yatawafika, kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi; naye atamlipa aliyetenda ibada yake vizuri na akajumuisha kati ya kuamini na kutenda mema kwa kumuingiza katika vyumba vya kifahari vyenye kila kitu ambayo roho zinavitamani, na macho yanavifurahia, nanyi mtadumu humo milele. Basi ni malipo mazuri zaidi Nyumba hizo katika Bustani za mbinguni kwa wale wanaomfanyia Mwenyezi Mungu matendo. "Ambao walisubiri" katika kumuabudu Mwenyezi Mungu "na wakamtegemea Mola wao Mlezi." katika kufanya hivyo. Kwa hivyo, uvumilivu wao katika kumuabudu kunalazimu kufanya bidii na kuweka nguvu katika kufanya hivyo, na kupigana vikali na Shetani, ambaye anawaita ili wakiuke kitu katika ibada hizo. Na kumtegemea kwao Mwenyezi Mungu kunalazimu ukubwa wa kumtegemea kwao, na dhana yao nzuri kwake kwamba atawawezesha kufikia yale waliyoyaazimia miongoni mwa matendo kuyakamilisha. Mwenyezi Mungu alitaja kutegemea haswa ingawa kunaingia katika subira kwa sababu hilo linahitajika katika kila kitendo, na kuacha kilichokatazwa, na hayo hayatimii isipokuwa kwa subira.