Al-Baqara
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
لِّلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِن نِّسَآئِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِن فَآءُو فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ 226
{226} Na hivi ni katika viapo mahususi kwa mke, katika jambo maalum, ambalo ni kiapo mumewe kuapa kuacha kumjamii mkewe kabisa, au kwa kuweka muda wa chini ya miezi minne au zaidi. Kwa hivyo, anayeapa kuacha kumjamii mkewe hasa, basi ikiwa ni chini ya miezi minne, hicho kitakuwa mfano wa viapo vinginevyo tu. Akikivunja kiapo chake, atatoa fidia. Na akikitimiza kiapo chake, basi hakuna chochote juu yake, na mkewe hana njia juu yake, kwa sababu amejizuia kwa muda wa miezi minne. Na ikiwa ni cha kuendelea milele, au kwa muda wa zaidi ya miezi minne, basi atapewa muda wa miezi minne katika kiapo chake, ikiwa mke wake atataka hivyo. Kwa sababu hiyo ni haki yake. Na muda huo ukiisha, ataamrishwa kumrudia, yani kujamii. Na akimjamii, basi hakuna kitu juu yake isipokuwa fidia ya kiapo. Na akikataa, atalazimishwa kumtaliki. Na akikataa, hakimu atamtalikia. Hata hivyo, kumrudia mkewe ndiko kunakopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ndiyo maana akasema: “Na wakirejea”yani kuachana na yale waliyoapa kuyaacha, nako ni kujamii. “Basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe” Anawasamehe kwa yale yaliyotokea kwa kuapa kwa sababu ya kurudi kwao. “Mwenye kurehemu,” kwa maana aliviwekea fidia viapo vyao, na cha kuwaondoa katika hilo, wala hakuvilazimisha juu yao, ambavyo haviwezekani kuvunjika. Na pia ni mwenye rehema juu yao kwa maana waliwarudia wake zao, na wakawahurumia na wakawarehemu.