Ibrahim
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
وَأَنذِرِ ٱلنَّاسَ يَوْمَ يَأْتِيهِمُ ٱلْعَذَابُ فَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ رَبَّنَآ أَخِّرْنَآ إِلَىٰٓ أَجَلٍ قَرِيبٍ نُّجِبْ دَعْوَتَكَ وَنَتَّبِعِ ٱلرُّسُلَ ۗ أَوَلَمْ تَكُونُوٓا۟ أَقْسَمْتُم مِّن قَبْلُ مَا لَكُم مِّن زَوَالٍ 44
{44} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad-rehema na amani za mwenyezi mungu zimshukie: "Na waonye watu siku itakapowajia adhabu" Yaani, waelezee maelezo ya hali hiyo, na watahadharishe matendo yanavyosababisha adhabu, adhabu ambayo inapokuja katika dhiki yake na wasiwasi wake, basi watasema wale waliodhulumu kwa ukafiri, ukadhibishaji na aina mbalimbali za maasia wakijutia yale waliyoyafanya, wakiomba kurejea katika wakati usiokuwa wakati wake, "Ewe Mola wetu Mlezi! Tuahirishe muda kidogo" Yaani: turudishe duniani. Kwa maana tumeshaona "tuitikie wito wako;" na Mwenyezi Mungu analingania kwenye nyumba ya salama, "na tuwafuate Mitume." Na haya yote ni kwa ajili ya kuokoka na adhabu chungu. Vinginevyo, wao ni waongo katika ahadi hii kwa maana lau watarudishwa, wangerejea katika yale waliyokatazwa, na ndiyo maana wanakemewa na kuambiwa: "Kwani nyinyi hamkuapa zamani kwamba hamtaondoka kamwe" katika dunia na kuhamia Akhera? Sasa anaglieni, imeshawabainikia kwamba mmevivunja viapo vyenu na mmedanganya katika hayo mliyodai.