پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
سورهٔ ۹

At-Tawba

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۰۸

لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا ۚ لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى ٱلتَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ ۚ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُوا۟ ۚ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلْمُطَّهِّرِينَ ۱۰۸

{108} "Usisimame ndani yake kabisa;” yaani, usiswalie kamwe katika msikiti huo ambao ulijengwa kwa ajili ya madhara. Mwenyezi Mungu atakutosheleza usiuhitaji, na wala hukulazimika kuswalia humo. "Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa uchamungu tangu siku ya mwanzo,” ambayo Uislamu uliingia Quba, nao ni Msikiti wa Quba uliosimamishwa juu ya msingi wa kumfanyia dini Mwenyezi Mungu tu na kusimamisha utajo wake na ibada mbalimbali za dini yake; na ulikuwa ni wa kale na mkuu katika hili. Basi Msikiti huu mbora "unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake,” na uabudu na umtaje Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi huo ni bora, na watu wake ni bora, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawasifu kwa kauli yake: "Humo wamo wanaume wanaopenda kujitakasa” kutokana na madhambi, na wanaojitakasa kutokana na uchafu, na najisi, na hadathi. Na inavyojulikana ni kwamba mwenye kupenda kitu, ni lazima ajitahidi kwa ajili yake na kufanya bidii katika hicho anachokipenda. Na ni lazima kwamba wao walikuwa wanalijali sana jambo la kujisafisha kutokana na madhambi, na uchafu, na hadathi. Na ndiyo maana wakawa miongoni mwa wale waliotangulia kusilimu, na walikuwa wakiisimamisha Swala, na wakiidumisha jihadi pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake - na kusimamisha ibada za Dini, na miongoni mwa wale ambao walikuwa wakichunga kutokwenda kinyume nao ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Baada ya kuteremka Aya hii ikiwasifu, Nabii - rehema na amani zimshukie - akawauliza kuhusu kujisafisha kwao. Wakamwambia kwamba wanafuatisha mawe maji, kwa hivyo akawasifu kwa kitendo chao hicho. “Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaojitakasa” utakaso wa kimaana, kama vile kujiepusha na shirki na tabia mbaya, na utakaso wa kimwili, kama vile kuondoa najisi, na hadathi.