At-Tawba
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًۢا بَيْنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ مِن قَبْلُ ۚ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَآ إِلَّا ٱلْحُسْنَىٰ ۖ وَٱللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ ۱۰۷
{107} Kulikuwa na watu fulani miongoni mwa wanafiki katika watu wa Quba ambao walijijengea msikiti karibu na Msikiti wa Quba kwa nia ya kuleta madhara na fitina baina ya waumini, na wanautayarisha kwa ajili ya wale wanaoutarajia miongoni mwa wale wanaopigana na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, ili uwe ngome kwao wanapoihitaji. Basi Yeye Mtukufu akabainisha hizaya yao, na akaidhihirisha siri yao hiyo, kwa hivyo akasema: "Na wapo waliojenga msikiti kwa ajili ya madhara;” yaani, kwa ajili ya kuwadhuru Waumini na Msikiti wao ambao wanakusanyika ndani yake, "na ukafiri." Yaani, lengo lao katika hilo ni kufuru ikiwa wengine wanataka kuamini, "na kuwafarikisha Waumini.” Yaani, ili wagawanyike, na watengane, na watofautiane, "na pa kuvizia;” yaani, kuwaandalia "wale waliompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake hapo kabla.” Yaani kwa ajili ya kuwasaidia wale wanaopigana na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, wale ambao waliwahi kupigana naye, na uadui wao ukazidi, kama vile Abu Amir Ar-Rahib, ambaye alikuwa miongoni mwa watu wa Madina, na Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alipokuja Madina, naye akahamia Madina, akamkufuru Nabii, na alikuwa ni mwingi wa kuabudu katika zama za Ujinga (kabla ya Uislamu). Kwa hivyo akawaendea washirikina ili kuwaomba msaada katika kupigana na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake. – Pindi alipokosa alichokuwa anakitaka kutoka kwao, akamwendea Kaisari akidhani kuwa atamsaidia, lakini yeye aliyelaaniwa akaangamia njiani, na yeye na wanafiki walikuwa kwenye ahadi na kusaidiana. Na kilikuwa katika yale waliyomwandalia ni Msikiti wa madhara, lakini ufunuo ukataremka na hilo. Kwa hivyo, Nabii - rehema na amani zimshukie - akautumia wa kuubomoa na kuuchoma moto. Kwa hivyo, ukabomolewa na ukachomwa moto, na baada ya hapo ukawa mahali pa kutupa takataka. Yeye Mtukufu akasema baada ya kubainisha miongoni mwa nia zao potovu kuhusiana na msikiti huo: "Na bila ya shaka wataapa kwamba: Hatukukusudia” katika kuujenga "isipokuwa uzuri tu." Yaani, kuwafanyia ihsani wanyonge, na wale wasiojiweza, na vipofu. "Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao hakika ni waongo.” Basi ushahidi wa Mwenyezi Mungu dhidi yao ni wa kweli zaidi kuliko viapo vyao hivyo.