Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأْتِيَهُمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ أَوْ يَأْتِىَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِىَ بَعْضُ ءَايَـٰتِ رَبِّكَ ۗ يَوْمَ يَأْتِى بَعْضُ ءَايَـٰتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَـٰنُهَا لَمْ تَكُنْ ءَامَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِىٓ إِيمَـٰنِهَا خَيْرًا ۗ قُلِ ٱنتَظِرُوٓا۟ إِنَّا مُنتَظِرُونَ ۱۵۸
{158} Yeye Mtukufu Anasema: Je, wanangoja hawa ambao imeendelea dhulma yao na ukaidi wao "isipokuwa kwamba wajiwe" na utangulizi wa adhabu, na utangulizi wa Akhera; ya kwamba wajiwe na "Malaika" ili kuchukua roho zao? Lakini wao wakifikia hali hiyo, haitawafaa kitu Imani yao wala mema ya matendo "au awajie Mola wako Mlezi" ili kupitisha hukumu baina ya waja na kuwalipa wafanyao mazuri na wafanyao mabaya "au ziwajie baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi?" Zinazoashiria ukaribu wa Saa (ya Qiyama). "Siku zitakapowajia baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi" ambazo si za kawaida, ambazo itajulikana kwazo kwamba Saa (ya Qiyama) imekwisha karibia na kwamba Qiyama kimeshakaribia; "kuamini kwa nafsi hapo hakutaifaa kitu, ikiwa haikuwa imeamini kabla yake, au imefanya heri katika Imani yake." Yaani, zikipatikana baadhi ya Ishara za Mwenyezi Mungu, basi kuamini kwa kafiri hakutamfaa ikiwa ataamini, wala Muumini anayepuuza kuzidishia heri baada ya hilo. Bali imani aliyokuwa nayo tu kabla ya hapo ndiyo itakayomnufaisha, na kheri aliyokuwa nayo kabla ya kuja kwa baadhi ya ishara hizo. Na hekima katika hili iko dhahiri. Nayo ni kwamba, imani ilikuwa yenye kunufaisha ikiwa ni kuamini ya ghaibu, na ikiwa ni kwa hiari ya mja. Ama zikipatikana Aya, basi jambo hilo linakuwa la wazi wazi, na imani haibaki kuwa na faida yoyote tena. Kwa sababu inafanana na imani ya lazima, kama vile imani ya mtu anayezama, na anayechomwa kwa moto, na mfano wake miongoni mwa yule ambaye akiona kifo, anaacha kile alichomo. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na walipoiona adhabu yetu, walisema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni wa pekee, na tumevikufuru vile tulivyokuwa tukimshirikisha navyo. Lakini imani yao hiyo haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati walipoiona adhabu yetu. Hii ndiyo ada ya Mwenyezi Mungu ambayo ilikwisha pita kwa waja wake." Na hadithi nyingi sahihi zilikuja kutoka kwa Nabii - rehema na amani zimshukie - kwamba kinachomaanishwa na baadhi ya Aya za Mwenyezi Mungu ni kuchomoza kwa jua kutokea magharibi yake, na kwamba watu watakapoliona; wataamini, lakini imani yao hiyo haitawafaa, kisha hapo mlango wa toba utafungwa. Na kwa kuwa hii ni ahadi ya adhabu kwa wanaomkadhibisha Mtume – rehema na amani zimshukie – anayoingoja, nao pia wanamngojelea Nabii – Rehema na Amani zimshukie – na wafuasi wake kuja kwa shida za wakati, na masaibu ya mambo. Akasema, “Sema: Ngojeni, nasi hakika pia ni wenye kungoja." Kisha mtakuja jua ni nani wetu anayestahiki zaidi amani. Na katika Aya hii kuna ushahidi wa dhehebu la Ahlus-Sunna Wal-Jamaa katika kuthibitisha matendo ya hiari ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama vile Al-Istiwaa (kukaa sawasawa), kushuka, na kuja kwa mwenyezi Mungu, mwingi wa baraka, Mtukufu bila ya kumfananisha na sifa za viumbe. Na katika Kitabu (yani Qur-aani) na Sunnah yako mengi katika haya. Na ndani yake pia ni kwamba miongoni mwa alama za Saa ni kuchomoza jua kutokea magharibi yake. Na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye hekima kubwa, na ni desturi yake na ada yake kwamba imani ina faida tu ikiwa ni ya hiari na si ya lazima, kama ilivyotangulia hapo awali. Na kwamba mtu anachuma heri kwa imani yake. Kwa hivyo Utii, na wema, na uchamungu hunufaisha na kukua iwapo mja ana imani. Lakini Ikiwa moyo wake hautakuwa na imani, basi Hatanufaishwa na chochote katika hayo.