Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَوْ تَقُولُوا۟ لَوْ أَنَّآ أُنزِلَ عَلَيْنَا ٱلْكِتَـٰبُ لَكُنَّآ أَهْدَىٰ مِنْهُمْ ۚ فَقَدْ جَآءَكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ وَصَدَفَ عَنْهَا ۗ سَنَجْزِى ٱلَّذِينَ يَصْدِفُونَ عَنْ ءَايَـٰتِنَا سُوٓءَ ٱلْعَذَابِ بِمَا كَانُوا۟ يَصْدِفُونَ ۱۵۷
{157} "Au mkasema: Lau hakika sisi tungeteremshiwa Kitabu hicho, basi tungelikuwa waongofu zaidi kuliko wao." Yaani, ima muweke udhuru kwamba hamkufikiwa na msingi wa uwongofu, au ima muweke udhuru wa kutokamilika kwake na kutokuwa kwake timilifu. Lakini mlipata kupitia kitabu chenu msingi wa uwongofu na ukamilifu wake, na ndiyo maana akasema: "Basi hakika imekwisha wajia hoja iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Na hili ni jina lenye kujumuisha vitu vya aina moja ambalo kinaingia ndani yake kila chenye kubainisha haki, "na uwongofu" kutokana na upotofu, "na rehema." Yaani, furaha kwenu katika dini yenu na dunia yenu. Basi hili linawalazimu kufuata hukumu zake na kuziamini habari zake, na kwamba asiyechukulia hayo kwa uzito na akayakadhibisha, basi hakika yeye ndiye dhalimu zaidi wa madhalimu wote. Na ndiyo maana akasema, "Kwa hivyo, ni nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayekadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo?" Yaani, alipeana mgongo na kujitenga upande. "Tutawalipa wale wanaojitenga na Ishara zetu adhabu mbaya kabisa." [Yaani, adhabu] ambayo ni mbaya kwa mwenyewe na ni ngumu kwake, "kwa sababu ya walivyokuwa wakijitenga" wao wenyewe na wengineo kama malipo kwao kwa matendo yao mabaya, na Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja wake kamwe. Na katika aya hizi kuna ushahidi kwamba, elimu ya Qur-aani ndiyo elimu tukufu zaidi, iliyobarikiwa yake zaidi, na ni pana yake zaidi, na kwamba kupitia kwayo unapatikana kuongoka kwenye njia iliyonyooka uwongofu timilifu usiohitaji pamoja nao kukisia kwa wanatheolojia, wala fikira za wanafalsafa, wala zisizokuwa hiyo miongoni mwa elimu za wa mwanzo na wa mwisho. Na kwamba inajulikana kuwa aina ya kitabu hicho haikuteremka isipokuwa kwa makundi mawili tu; ya Mayahudi na Wakristo. Basi Hao ndio watu wa Kitabu kwa jumla, na wala hayaingii ndani yao makundi mengine yote, si Mamajusi wala wasiokuwa wao. Na ndani yake ni kuwa hali waliyokuwamo watu wa zama za ujinga kabla ya kuteremka kwa Qur-aani miongoni mwa ujinga mkubwa na kutokuwa na elimu ya yale waliyokuwa nayo Watu wa Kitabu ambao wana kiini cha elimu, na kughafilika kwao kusoma vitabu vyao.