Al-An'aam
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِذَا جَآءَتْهُمْ ءَايَةٌ قَالُوا۟ لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَآ أُوتِىَ رُسُلُ ٱللَّهِ ۘ ٱللَّهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُۥ ۗ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ أَجْرَمُوا۟ صَغَارٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌۢ بِمَا كَانُوا۟ يَمْكُرُونَ ۱۲۴
{124} Lakini wahalifu wakubwa walibakia katika batili yao, na wakaikanusha haki ambayo walikuja nayo Mitume kwa ajili ya husuda yao na uadui. Kwa hivyo wakasema: "Hatutaamini mpaka tupewe mfano wa yale waliyopewa Mitume wa Mwenyezi Mungu" miongoni mwa unabii na utume. Na katika hayo kuna upinzani wao dhidi ya Mwenyezi Mungu, na kujiona, na kuifanyia kiburi haki ambayo aliiteremsha juu ya mikono ya mitume wake, na kujizuia fadhila ya Mwenyezi Mungu na ukarimu wake. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawajibu pingamizi lao potovu, na akajulisha kuwa hawaifailii heri, wala hawana ndani yao chenye kufanya wawe miongoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu, achilia mbali kwamba wawe miongoni mwa Manabii na Mitume. Ndiyo akasema: "Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi ni wapi anauweka ujumbe wake." Kwa hivyo Yeyote yule anayemjua kuwa anafaa kwa hilo, na atatekeleza majukumu yake, huku akiwa anasifika na kila tabia nzuri, anayejiweka mbali na kila tabia mbaya, basi Mwenyezi Mungu atampa kile ambacho hekima yake inakihitaji katika asili na matokeo yake. Na asiyekuwa hivyo, hataweka tunu zake bora zaidi kwa yule ambaye hazistahili na si mtakatifu kwake. Na katika Aya hii kuna ushahidi wa ukamilifu wa hekima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sababu, hata ikiwa Yeye Mtukufu ni Mwenye kurehemu, na Mwenye kupeana kwa wingi, mwingi wa ihsani, basi yeye hakika ni mwenye hekima kubwa, na haweki ukarimu wake isipokuwa kwa anayeustahili. Kisha akaahidi wahalifu adhabu, akisema: “Itawafikia wale waliofanya uhalifu udhalili kwa Mwenyezi Mungu.” Yaani, kudunishwa na udhalilifu. Kama vile walivyoifanyia haki kiburi, basi Mwenyezi Mungu aliwadhalilisha "na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya." Yaani, kwa sababu vitimbi vyao, si kwa sababu ya Yeye Mtukufu kuwadhulumu.