Al-Mujaadila
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ تَوَلَّوْا۟ قَوْمًا غَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مَّا هُم مِّنكُمْ وَلَا مِنْهُمْ وَيَحْلِفُونَ عَلَى ٱلْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ۱۴ أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ إِنَّهُمْ سَآءَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ۱۵
{14 - 15} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu ubaya wa hali ya wanafiki, ambao ni washirika wanafanya urafiki wendani na makafiri miongoni mwa Mayahudi, Wakristo, na wengineo ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia na wakapokea fungu kamili katika laana ya Mwenyezi Mungu, na ya kwamba wao si miongoni mwa Waumini wala miongoni mwa makafiri. “Wanayumba yumba baina ya huku na huko. Huku hawako, na huko hawako.” Wao si Waumini kwa dhahiri wala kwa ndani, kwa sababu kwa ndani yao wako pamoja na makafiri, na wala hawako pamoja na makafiri kwa dhahiri na kwa ndani. Kwa sababu kwa dhahiri yao wako pamoja na Waumini. Hii ndiyo sifa yao ambayo Mwenyezi Mungu amewaelezea kwayo, na hali ni kuwa wanaapa kwa kinyume chake, ambacho ni kusema uongo. Wanaapa kwamba wao ni Waumini, na hali ni kwamba wao sio Waumini. Basi malipo ya wahaini hawa, waovu na waongo ni kwamba Mwenyezi Mungu amewaandalia adhabu kali ambayo haiwezi kukadiriwa kiasi chake wala hata maelezo yake hayajulikani: “Kwa hakika waliyokuwa wakiyatenda ni maovu kabisa.” Kwa maana walifanya yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu na yanawasababishia kupata adhabu na laana.