پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Mujaadila
سورهٔ ۵۸

Al-Mujaadila

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۳

ءَأَشْفَقْتُمْ أَن تُقَدِّمُوا۟ بَيْنَ يَدَىْ نَجْوَىٰكُمْ صَدَقَـٰتٍ ۚ فَإِذْ لَمْ تَفْعَلُوا۟ وَتَابَ ٱللَّهُ عَلَيْكُمْ فَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ ۚ وَٱللَّهُ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ ۱۳

{13} Basi [Mwenyezi Mungu, Mwenye baraka nyingi] Mtukufu alipoona huruma kubwa ya Waumini na ugumu wa kuwatolea sadaka wakati wa kumnong’onezea Mtume, akawafanyia jambo hilo kuwa jepesi, na wala hakuwachukulia makosa ya kuacha kutoa sadaka kabla ya kumnong’onezea, kukabakia kumheshimu Mtume na kumpa taadhima kama ilivyo bila ya kufutwa. Kwa sababu [hukumu] hii katika hukumu zilizowekwa si kwa ajili yake yenyewe. Bali kilichokusudiwa ni kuwa na adabu nzuri mbele ya Mtume na kumheshimu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaamrisha kutekeleza maamrisho makubwa yaliyokusudiwa yenyewe. Akasema: “Ikiwa hamkufanya hayo.” Yaani, ikiwa si rahisi kwenu kutoa sadaka, lakini hili halitoshi. Kwani si sharti la jambo kuwa lazima kwamba liwe jepesi kwa mja, na ndiyo maana akaliwekea mipaka kwa kusema: “Na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu.” Yaani, akakusameheni hilo, basi shikeni Sala” kwa kutekeleza nguzo zake, masharti yake, na mipaka yake na mambo yote yanayofungamana nayo. “Na toeni Zaka” ya lazima kutoka katika mali zenu na muwape wale wanaostahiki kupewa. Ibada hizi mbili ndizo mama ya ibada za kimwili na za kimali. Kwa hivyo, mwenye kuzitekeleza ipasavyo kisheria, basi atakuwa ametekeelza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, na ndiyo maana akasema baada yake: “Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Na hii ndiyo amri inayojumuisha zaidi, kwa hivyo inaingia humo kumtii Mwenyezi Mungu na kumtii Mtume wake kwa kutekeleza maamrisho yao, kujiepusha na makatazo yao, kusadiki waliyotuambia, kusimamia kwenye mipaka ya Sheria, na kinachozingatiwa zaidi katika hayo ni kumkusudia Mwenyezi Mungu tu na kufanya mambo kwa uzuri zaidi. Ndiyo maana akasema: “Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.” Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anayajua matendo yenu, na kwa namna gani yalifanyika, kisha atawalipa kulingana na anavyojua yale yaliyomo vifuani mwao.