Al-Mujaadila
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُوا۟ فِى ٱلْمَجَـٰلِسِ فَٱفْسَحُوا۟ يَفْسَحِ ٱللَّهُ لَكُمْ ۖ وَإِذَا قِيلَ ٱنشُزُوا۟ فَٱنشُزُوا۟ يَرْفَعِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ دَرَجَـٰتٍ ۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ۱۱
{11} Hii ni adabu nzuri ambayo Mwenyezi Mungu anawafunza waja wake wanapokuwa wamekusanyika katika mkusanyiko yao, wakati baadhi yao watahitaji kusongewa. Basi ni katika adabu nzuri kwamba afanyiwe nafasi, na hilo halimdhuru mwenye kusonga akatengeneza nafasi kwa chochote, akawa huyo ndugu yake amefikia lengo lake bila ya yeye kufikiwa na madhara yoyote, na malipo ni ya aina sawa na matendo. Kwa sababu, mwenye kusonga akatengeneza nafasi, Mwenyezi Mungu anamfanyia nafasi. Na mwenye kumpanulia ndugu yake, Mwenyezi Mungu anampanulia. “Na mkiambiwa: Ondokeni” Yaani, simameni na jitengeni na mikusanyiko yenu kwa sababu ya haja fulani inayojitokeza, “basi ondokeni.” Yaani, harakisheni kunyanyuka ili kufikia masilahi hayo. Kwani, kufanya mambo hayo ni katika elimu na imani, na Mwenyezi Mungu Mtukufu huwanyanyua watu wa elimu na imani kwa daraja mbalimbali kulingana elimu ambayo [Mwenyezi Mungu] aliwapa. “Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.” Kisha atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake. Yakiwa ni mazuri, basi kwa uzuri. Na ikiwa ni mabaya, basi kwa ubaya. Katika Aya hii, kuna fadhila ya elimu, na pambo lake na matunda yake ni kuwa na adabu zake na kutenda kulingana na matakwa yake.