پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
سورهٔ ۵

Al-Maaida

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیه‌های ۹۰–۹۱

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّمَا ٱلْخَمْرُ وَٱلْمَيْسِرُ وَٱلْأَنصَابُ وَٱلْأَزْلَـٰمُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ ٱلشَّيْطَـٰنِ فَٱجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ۹۰ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱلشَّيْطَـٰنُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ ٱلْعَدَٰوَةَ وَٱلْبَغْضَآءَ فِى ٱلْخَمْرِ وَٱلْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ ٱللَّهِ وَعَنِ ٱلصَّلَوٰةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ۹۱

{90 - 91} Yeye Mtukufu anavishutumu vitu hivi vibaya, na anajulisha kwamba hivyo ni katika kazi ya Shetani, na kwamba ni vichafu. "Basi jiepusheni navyo;" yaani viacheni, "ili mfaulu;" kwa maana, kufaulu hakutimii isipokuwa kwa kuacha yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, hasa hivi vichafu vilivyoyataja; navyo ni mvinyo. Nayo ni kila chenye kufunika akili kwa kuilewesha. Na Maisir, ambayo ni ushindi wote ambao ndani yake kuna malipo kutoka pande zote mbili, Kama vile kamari na mfano wake. Na Answaab, ambayo ni masanamu na waungu, na mfano wake miongoni mwa vinavyosimamishwa na kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu. Al-Azlaam [ambazo wanaapa kwazo]. Basi hivi vinne Mwenyezi Mungu amevikataza, na akakemea dhidi yake, na akajulisha maharibifu yake, yenye kufanya mtu kuyaacha na kuyaepuka. Miongoni mwake ni kwamba vichafu. Yaani, viachafu kimaana, hata ikiwa si najisi kihisia. Na vitu vichafu ni miongoni mwa yale yanayopasa kuyaepuka, na kutojichafua na uchafu wake. Na miongoni mwake ni kwamba, ni katika kazi ya Shetani, ambaye ndiye adui mkubwa zaidi ya maadui wote wa mwanadamu. Na inajulikana ni kwamba adui anaepukwa, inaepukwa mitego yake, na matendo yake, hasa matendo yale ambayo anafanya ili kumnasa adui yake. Kwa maana ndani yake kuna kuangamia kwake. Basi na liazimiwe kila azimio kuwa mbali na vitendo vya adui wa wazi, na kujitahadharisha navyo, na kuhofu kuanguka ndani yake. Na miongoni mwake ni kwamba, haiwezekani kwa mja kufaulu isipokuwa kwa kuviepuka. Kwa maana kufaulu ni kufuzu kufikia kinachotafutwa na kinachopendwa, na kuokoka kutoka katika kile kinachohofiwa. Na vitu hivi huzuia kufaulu. Na miongoni mwake ni kwamba, hivi vinasababisha uadui na chuki baina ya watu. Naye Shetani ana shauku kubwa ya kuvieneza, hasa mvinyo na kamari ili aweke uadui na chuki baina ya Waumini. Kwa maana katika mvinyo kuna kupinduka akili na kupoteza fahamu wake, jambo linalopelekea kuwepo chuki baina yake na ndugu zake miongoni mwa Waumini; hasa ikiambatana na hilo [matusi] ambayo hayaachani na mnywaji pombe. Hiyo huenda hata ikafikisha katika kuua. Na yale yaliyo katika kamari ya mmoja wao kumshinda mwenzake, na kuchukua mali yake nyingi bila ya kibadala chake, jambo ambalo ni moja ya sababu kubwa za uadui na chuki. Na miongoni mwake ni kwamba, vitu hivi vinauzuia moyo, kisha unafuatwa na mwili kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na kuswali, ambayo mja aliumbwa kwa ajili yake, na kwa mawili haya, ndiyo kuna furaha yake. Basi mvinyo na kamari humzuia sana na hayo kuzuia kukubwa zaidi. Na moyo wake unashughulika nayo, na akili yake inashughulika nayo, mpaka anapitwa na muda mrefu hali ya kuwa hajui yuko wapi. Basi ni maasia gani yaliyo makubwa zaidi na mabaya zaidi kuliko maasia yenye kumchafua mwenyewe, na yanamfanya kuwa katika watu wa machafu, na yanamuingiza katika matendo ya Shetani, na mitego yake? Kwa hivyo anamfuata kama vile mnyama mtiifu anavyofuata mchungaji wake, na yanazuia kati ya mja na kufaulu kwake, na yanasababisha uadui na chuki baina ya Waumini, na yanazuia kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali. Basi je, juu ya maharibifu haya kuna kitu kikubwa zaidi yake? Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akawaambia Waumini kwa njia isiyo ya moja kwa moja katazo juu ya hayo kwa kauli yake: "Basi je, mmeacha?" Kwa sababu mtu mwenye akili timamu akiangalia baadhi ya maharibifu hayo, anakomeka nayo, na kujizuia, na hahitaji kuwaidhiwa kwa wingi, wala karipio la kuingia ndani yake.