Al-Maaida
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
لَّقَدْ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ مَرْيَمَ ۚ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ مِنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا إِنْ أَرَادَ أَن يُهْلِكَ ٱلْمَسِيحَ ٱبْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُۥ وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا ۗ وَلِلَّهِ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ ۱۷
{17} Yeye Mtukufu alipotaja kuchukua agano kwa Watu wa Vitabu viwili, na kwamba hawakulisimamisha, bali walilivunja, akataja kauli zao za kuchukiza. Basi akataja kauli ya Wakristo, kauli ambayo hakuna mwingine aliyewahi kuisema asiyekuwa wao, kwamba Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryam. Na msingi wa tuhuma yao hii ni kuwa alizaliwa bila ya baba, basi wakaitakidi kuhusiana naye itikadi hii potofu, licha ya kuwa Hawa ni sawa na yeye, aliumbwa bila ya mama, na Adamu naye anastahiki zaidi kumliko, kwa sababu aliumbwa bila ya baba wala mama. Basi kwa nini hawakudai uungu katika hao kama walivyoudai katika Masihi? Kwa hivyo likaashiria kuwa kauli yao hii ni kufuata matamanio bila ya uthibitisho wala shaka yoyote. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawajibu kwa hoja za kiakili zilizo wazi, akasema, "Sema: Basi ni nani mwenye kumiliki chochote mbele ya Mwenyezi Mungu ikiwa Yeye angetaka kumwangamiza Masihi mwana wa Maryam, na mama yake, na wote waliomo katika ardhi?" Ikiwa waliotajwa hao hawana uwezo wa kuzuia ambao utawazuia ikiwa Mwenyezi Mungu atataka kuwaangamiza, na wala hawana uwezo wa kufanya hivyo, basi hilo linaashiria ubatili wa uungu wa yule ambaye hawezi kujiepusha na maangamivu, wala hana chochote katika uwezo wake kujinasua. Na miongoni mwa ushahidi ni kwamba, "ni wa Mwenyezi Mungu" peke yake "ufalme wa mbingu na ardhi." Anawaendesha kwa hukumu yake ya kiulimwengu, na ya kisheria, na ya kiadhabu. Nao wanamilikiwa na wanaendeshwa. Basi Je, inafaa kwa mja mmilikiwa maskini kuwa mungu anayeabudiwa, tajiri kwa kila namna? Hili ni miongoni mwa mambo makubwa yasiyowezekana, na wala hakuna sababu yoyote ya kustaajabu kwao kumuumba Masihi Isa bin Maryam bila ya baba. Kwani Mwenyezi Mungu "huumba apendavyo." Akipenda ni kutoka kwa baba na mama, kama vile watoto wengine wote wa Adam. Na akipenda ni kutoka kwa baba bila ya na mama, kama vile Hawa. Na akipenda ni kutoka kwa mama bila ya baba kama vile Isa. Na akitaka ni kwa bila ya baba wala mama kama vile Adam. Basi kuwepo aina tofauti za uumbaji wake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kulingana na mapenzi yake ambayo hakizuiliki kitu kwake. Na ndiyo maana akasema, "Na Mwenyezi Mungu ana uweza juu ya kila kitu."