پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
سورهٔ ۴

An-Nisaa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۹۷

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَفَّىٰهُمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ ظَالِمِىٓ أَنفُسِهِمْ قَالُوا۟ فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا۟ كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ قَالُوٓا۟ أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةً فَتُهَاجِرُوا۟ فِيهَا ۚ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ مَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَآءَتْ مَصِيرًا ۹۷

{97} Hii ni ahadi ya adhabu iliyo kubwa kwa mwenye kuacha kuhama ingawa ana uwezo wa kufanya hivyo mpaka akafa. Kwa maana, Malaika wanaoichukua roho yake wanamkaripia kwa karipio hili kubwa, na wanawaambia, “Mlikuwa katika?” Yani mlikuwa katika hali gani? Na ni kwa kitu gani mlikuwa toafuti na makafiri? Bali nyinyi mlizidisha idadi yao, na labda mliwaunga mkono dhidi ya Waumini, na mkakosa heri nyingi, na Jihadi pamoja na Mtume wake, kuwa pamoja na Waislamu, na kuwasaidia dhidi ya maadui zao. “Watasema: Tulikuwa tumefanywa kuwa wanyoge katika ardhi.” Yani tulikuwa dhaifu, wenye kukandamizwa, wenye kudhulumiwa, hatuna uwezo wa kuhama. Lakini wao si wakweli katika hilo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwakemea na akawaahidi adhabu. Na Mwenyezi Mungu haitwiki nafsi isipokuwa uwezo wake. Na aliwaondoa katika hilo wale waliofanywa kuwa wanyonge kikweli, na kwa sababu hiyo, Malaika wakawaambia, “Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa, mkahamie humo?” Na hili ni swali la kuwafanya wakiri. Yani kila mtu anakubali kwamba dunia ya Mwenyezi Mungu ni pana. Basi popote anapokuwa mja katika mahali ambapo hawezi kudhihirisha dini yake huko, ana nafasi ya kutosha katika ardhi ambapo anaweza kumwabudu Mwenyezi Mungu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, “Enyi waja wangu mlioamini! Kwa hakika ardhi yangu ni pana. Basi niabuduni Mimi peke yangu.” Mwenyezi Mungu alisema kuhusu hawa ambao hawana udhuru, “Basi hao makazi yao ni Jahannam, nayo ni marejeo mabaya kabisa.” Na hii ni kama ilivyotajwa hapo awali katika kuelezea sababu inayosababisha hilo. Inaweza kusababisha matakwa yake pamoja kuwepo kwa masharti yake na kutokuwepo kwa vizuizi vyake, na kinaweza kizuizi kingine kuzuia kufanya hivyo. Katika Aya hii kuna ushahidi ya kwamba kuhama ni miongoni mwa wajibu mkubwa, na kuuacha ni miongoni mwa mambo yaliyoharamishwa, bali ni katika madhambi makubwa zaidi. Na katika Aya hii kuna ushahidi kwamba kila mwenye kufa, basi amekwisha kamilisha na akatimiza yale aliyoandikiwa katika riziki, na muda wa uhai wake, na matendo, na hilo limechukuliwa kutoka kwenye neno “at-tawaffi;” kwa maana hilo linaliashiria hilo. Kwa sababu, ikiwa kingekuwa kimesalia chochote katika hayo, basi hangekuwa amekamilishiwa. Na ndani yake kuna kuwaamini Malaika na kuwasifu. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu aliyasema maneno hayo kwa niaba yao kwa njia ya kuyakubali na kupendekeza walichofanya, na kuona kuwa kinafaa.