An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
لَّا يَسْتَوِى ٱلْقَـٰعِدُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُو۟لِى ٱلضَّرَرِ وَٱلْمُجَـٰهِدُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ فَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلْمُجَـٰهِدِينَ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ عَلَى ٱلْقَـٰعِدِينَ دَرَجَةً ۚ وَكُلًّا وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلْحُسْنَىٰ ۚ وَفَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلْمُجَـٰهِدِينَ عَلَى ٱلْقَـٰعِدِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ۹۵ دَرَجَـٰتٍ مِّنْهُ وَمَغْفِرَةً وَرَحْمَةً ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ۹۶
{95 - 96} Yani hatoshani anayepigana Jihadi miongoni mwa Waumini kwa nafsi yake na mali yake na yule ambaye hakutoka kwenda katika jihadi na wala hakupigana na maadui wa Mwenyezi Mungu. Basi ndani yake kuna kuhimiza juu ya kutoka kwenda Jihadi, na kupeana moyo kuhusiana na hilo, na kuhofisha dhidi ya uvivu na kusalia nyuma yake bila ya udhuru. Ama wale wenye dharura, kama vile wagonjwa, na vipofu, na viwete, na asiyepata chochote cha kujiandaa kwacho. Basi hao hawako katika nafasi sawa na wale wanaokaa bila ya udhuru. Kwa hivyo, yeyote ambaye ni miongoni mwa wenye madhara na akaridhika na kukaa kwake, na asikusudie kutoka katika njia ya Mwenyezi Mungu, lau kuwa madhara hayo hayangekuwepo, na wala hajiambii nafsi yake juu ya hilo, basi yeye yuko katika nafasi ya yule aliyekaa bila udhuru. Na yeyote ambaye anaazimia kutoka kwenda katika Njia ya Mwenyezi Mungu lau si tu kwa sababu ya kuwepo kwa kizuizi anatamani hilo na anajiambia nafsi juu ya hilo, basi yeye yuko katika nafasi ya mwenye kutoka kwenda katika jihadi. Kwa sababu, nia thabiti inaposhikana na kile inachoweza kama vile kauli au kitendo, basi mwenye hilo atawekwa katika daraja ya aliyefanya hasa. Kisha Yeye Mtukufu akasema waziwazi kwamba aliwaboresha kwa daraja wale wanaopigana juu ya wale wanaosalia nyuma. Na huku ni kuboresha kwa ujumla. Kisha akasema hilo waziwazi kwa kina, na akawaahidi kufutiwa dhambi kutoka kwa Mola wao Mlezi na rehema ambazo zinajumuisha kupata heri yote na kuzuilika kwa maovu yote, na daraja ambazo Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, –alizifafanua kwa hadithi iliyothibitika kutoka kwake katika Sahih Mbili, “Hakika, katika Pepo kuna daraja mia moja. Umbali wa baina ya kila daraja mbili ni kama umbali wa kati ya mbingu na ardhi. Mwenyezi Mungu aliziandaa kwa ajili ya wale wanaopigania katika Njia yake.” Na thawabu hizi ambazo Mwenyezi Mungu ameziweka kwa ajili ya jihadi ni sawa na yale yaliyomo katika Sura Al-Saff katika kauli yake. “Enyi mlioamini! Je, niwaonyeshe biashara itakayowaokoa kutokana na adhabu chungu? Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu. Hayo ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua. Atawafutia dhambi zenu, na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito chini yake, na maskani mazuri mno katika Bustani za milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa....” mpaka mwisho wa surah. Na tafakari uzuri wa kubadilika kutoka katika hali moja hadi katika hali nyingine ya juu kuiliko. Kwanza, alikanusha usawa baina ya wanaopigana Jihadi na wengineo, kisha akasema waziwazi kwamba amewaboresha kwa daraja wanaopigana Jihadi juu ya wanaosalia nyuma. Kisha akaelekea katika kumboresha kwa kufutiwa dhambi, na rehema, na daraja mbalimbali. Na huku kutoka katika hali moja hadi katika hali nyingine ya juu kuiliko wakati wa kuboresha, na kusifu, au kushuka kutoka katika hali moja hadi katika hali nyingine ya chini yake wakati wa kukashifu na kulaumu ni maneno bora zaidi na ya kugusa zaidi nafsi. Na vile vile anapokiboresha Yeye Mtukufu kitu juu ya kitu, na kila moja yake ina fadhila, anatahadhari kwa kutaja fadhila inayojumuisha mambo mawili hayo ili asije mtu akawaza vibaya kwamba yule ambaye hakuboreshwa analaumiwa, kama alivyosema hapa. “Na kila mmoja wao Mwenyezi Mungu amemuahidi mazuri.” Na kama alivyosema Yeye Mtukufu katika Aya zilizotajwa katika Surat Assaff katika kauli yake, “na wape Waumini bishara njema” na kama alivyosema katika kauli yake, “Hawawi sawa miongoni mwenu wale waliotoa kabla ya Ushindi na wakapigana vita,” yani kuliko yule ambaye hakuwa hivyo. Kisha akasema, “Na kila mmoja wao Mwenyezi Mungu amemuahidi mazuri.” Na kama alivyosema Yeye Mtukufu, “Kwa hivyo, tukamfahamisha Suleimani hilo. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na elimu.” Basi inampasa yule anayetafiti katika kuboresha baina ya watu, na kazi, na matendo kwamba alifahamu jambo hili muhimu. Na kadhalika, ikiwa alizungumza kuhusu kutaja sifa mbaya za watu na makala, ataje kile ambacho vinajumuika ndani yake wakati wa kuboresha baadhi yake kuliko nyingine, ili isije ikafikiriwa vibaya kuwa yule ambaye hakuboreshwa amepata ukamilifu. Kama ikisemwa: Wakristo ni bora kuliko Majusi. Basi na aseme pamoja na hilo: Na kila mmoja wao ni kafiri. Na kuua ni kubaya zaidi kuliko zinaa, na kila moja yake ni dhambi kubwa ambayo Mwenyezi Mungu ameiharamisha na Mtume wake, akaikemea. Na alipowaahidi wanopigana Jihadi kufutiwa dhambi, na rehema vitokanavyo na majina yake mawili matukufu, ‘Mwingi wa kufuta dhambi’ na ‘Mwenye kurehemu’, akaimalizia Aya hii kwa kusema; “Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi mno, na Mwenye kurehemu sana.”