An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ جَآءُوكَ فَٱسْتَغْفَرُوا۟ ٱللَّهَ وَٱسْتَغْفَرَ لَهُمُ ٱلرَّسُولُ لَوَجَدُوا۟ ٱللَّهَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ۶۴
{64} Yeye Mtukufu anajulisha habari ambazo ndani yake kuna amri na kuhimiza juu ya kumtii Mtume na kumfuata. Na kwamba makusudio ya kuwatuma Mitume ni wao kutiiwa, na kufuatwa na wale waliotumiwa (Manabii hao) katika kila waliyoamrisha na waliyokataza. Na kwamba waheshimiwe kama vile yule anayetii humheshimu yule anayemtii. Na katika hili kuna kuthibitisha kuhifadhiwa kwa Mitume katika yale wanayofikisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na katika yale wanayoamrisha na kukataza. Na kwa sababu Mwenyezi Mungu aliamrisha watiiwe kabisa. Na lau si kwamba wao wamehifadhiwa, na kwamba hawaweki sheria ambayo ni makosa, basi hangeamrisha hilo kabisa. Na kauli yake, "kwa idhini ya Mwenyezi Mungu." Yani utiifu kutoka kwa mtiifu unatokana na hukumu ya Mwenyezi Mungu na majaaliwa yake. Basi ndani yake kuna uthibitisho wa hukumu ya Mwenyezi Mungu na majaaliwa yake, na kuhimiza kutafuta msaada wa Mwenyezi Mungu, na kubainisha kwamba mtu hawezi kumtii Mtume ikiwa Mwenyezi Mungu hatamsaidia. Kisha akaeleza kuhusu ukarimu wake mkubwa, upaji wake mkubwa, na kumlingania kwake yule aliyefanya maovu kwamba wakubali, na watubie, na wamwombe Mwenyezi Mungu kuwafutia dhambi. Akasema, "Na lau pale walipozidhulumu nafsi zao wangelikujia," yani, hali ya kuwa wamezikubali dhambi zao na kusononeka juu yake. "Hivyo wakamwomba Mwenyezi Mungu kuwafutia dhambi, na Mtume akawaombea kufutiwa dhambi, basi bila ya shaka wangelimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu." Yani angewakubalia toba yao kwa kuwafutia dhambi za dhuluma yao, na akawarehemu kwa kuwakubalia toba yao, na kuwawezesha kuifikia, na kuwalipa juu yake. Na kuja huku kwa Mtume -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ni mahsusi katika siku za uhai wake. Kwa sababu, muktadha unaonyesha hilo. Kwa sababu, kuomba istighfari kwa Mtume hakuwi isipokuwa wakati wa uhai wake. Na ama baada ya kufa kwake, haombwi kitu, bali hilo ni shirki.