An-Nisaa
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُم ۚ بَلِ ٱللَّهُ يُزَكِّى مَن يَشَآءُ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا ۴۹
{49} Huku ni kustaajabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na ni karipio kwa wale wanaojitakasa nafsi zao miongoni mwa Mayahudi na Wakristo, na wale wanaowafuata mfano wao katika kila anayejitakasa nafsi yake kwa jambo lisilokuwa ndani yake. Na hilo ni kwamba Mayahudi na Wakristo husema, "Sisi ni wana wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake." Na husema, "Hataingia Peponi ila aliyekuwa Myahudi au Mkristo." Na haya ni madai matupu tu ambayo hayana ushahidi wowote juu yake. Lakini ushahidi ni yale yaliyoelezwa katika Qur-ani katika kauli yake, "Sivyo hivyo! Yeyote anayeuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu naye ni mtenda mema, basi ana malipo yake kwa Mola wake Mlezi, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika." Basi hao ndio aliowatakasa Mwenyezi Mungu, na ndiyo maana akasema hapa, "Bali Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye." Yani kwa imani na matendo mema, kwa kuacha tabia mbovu na kujipamba kwa sifa nzuri. Na ama hawa, basi hao hata wakijitakasa nafsi zao kwa kudai kwao kuwa wako juu ya kitu, na kwamba thawabu ni zao peke yao. Hao kwa hakika ni waongo katika hilo, na hawana fungu katika sifa za waliotakasika, kwa sababu ya dhuluma yao na ukafiri wao, na si kwa Mwenyezi Mungu kuwadhulumu. Na ndiyo maana akasema, "Na hawatadhulumiwa hata kiasi cha kijiuzi kilichomo ndani ya uwazi wa kokwa ya tende." Na hili ni kufikia ujumla. Yani hawatadhulumiwa kitu, hata kiasi cha Fatiil ambayo iko kwenye uwazi wa kokwa ya tende, au ile inayopulizwa katika uchafu wa mkononi na vinginevyo.