پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Ar-Room
سورهٔ ۳۰

Ar-Room

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۳۲

مِنَ ٱلَّذِينَ فَرَّقُوا۟ دِينَهُمْ وَكَانُوا۟ شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍۭ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ ۳۲

{32} Kisha akataja hali ya washirikina na kuonyesha uduni wake na ubaya wake. Akasema, "Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao," ijapokuwa Dini ni moja, ambayo ni kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika ibada. Na washirikina hawa waliigawanya: miongoni mwao wapo wanaoabudu masanamu, na miongoni mwao wapo wanaoabudu jua na mwezi, na miongoni mwao wapo wanaoabudu mawalii (watu walio karibu na Mwenyezi Mungu) na watu wema, na miongoni mwao wapo Mayahudi, na miongoni mwao wapo Wakristo. Na ndiyo maana akasema, "Na wakawa makundi makundi." Yaani, kila kundi miongoni mwa washirikina wakapotea na wakawa washabiki katika kuunga mkono batili waliyo nayo, na kuwapinga wengineo na kuwapiga vita. "Kila kikundi kinafurahia kilicho nacho" cha elimu mbalimbali iliyo kinyume na elimu ya Mitume na kwayo wanajihukumu wenyewe kuwa hiyo ndiyo haki na kwamba wengineo wako katika batili. Na katika hilo kuna hatadharisho kwa Waislamu dhidi ya kutawanyika na kutengana makundi makundi, kila kundi likawa linatetea yale waliyo nayo ya haki na batili, kwa hivyo wakawa wamefanana na washirikina katika kugawanyika kwao. Bali Dini ni moja, Mtume ni mmoja, na Mwenyezi Mungu ni mmoja, na katika mambo mengi ya kidini kuna maafikiano baina ya wanachuoni na maimamu, na udugu wa kiimani ulikwisha wekwa na Mwenyezi Mungu na akaufunga vyema kabisa. Basi kwa nini yote haya yanafutwa na unajengwa mgawanyiko na fitina baina ya Waislamu juu ya mambo yaliyofichikana au masuala ya kimatawi yenye utata ambayo kwayo wao kwa wao wanaonana kwamba kila mmoja wao amepotea, na wanajitofautisha baadi yao kutoka kwa wengineo? Je, huu si isipokuwa uchochezi mkubwa wa Shetani na malengo yake makubwa zaidi ambayo kwayo anawapangia njama Waislamu? Je, kujitahidi kuunganisha neno lao na kuondoa tofauti hizi zilizo baina yao zilizojengeka juu ya msingi huo batili, si isipokuwa ndiyo jihadi bora zaidi katika njia ya Mwenyezi Mungu na matendo bora zaidi yanayomuweka mtu karibu na Mwenyezi Mungu? Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoamuru kutubia kwake, na kukawa kutubia huko ni kule kwa hiari, ambako kunakuwa katika hali ya shida, na urahisi, na wingi na dhiki, akataja kutubia kwa kulazimishwa ambako hutokea mtu isipokuwa wakati anapokuwa katika shida na dhiki. Na pindi dhiki hiyo inapomuondokea, anaitupa nyuma ya mgongo wake, lakini toba hii hainufaishi kitu. Akasema: