Ar-Room
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ ٱللَّهِ ٱلَّتِى فَطَرَ ٱلنَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ۳۰
{30} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamrisha kwamba akusudiwe Yeye tu katika kila hali na kuisimamisha Dini yake. Alisema, "Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini" ambayo ni Uislamu, Imani, na ihsani, kwa kuelekeza moyo wako, nia yako, na mwili wako katika kusimamisha sheria dhahiri za Dini, kama vile swala, zaka, saumu, Hijja, na mfano ya hayo, na sheria zake zilizofichika, kama vile upendo, hofu, matumaini, kurudi kwa Mwenyezi Mungu, na kufanya kwa uzuri sana sheria zilizo wazi na zilizofichikana; kwa kumwabudu Mwenyezi Mungu ndani yake kana kwamba unamwona. Na ikiwa hamuoni; basi hakika Yeye anakuona. Na hapa Mwenyezi Mungu aliamrisha kuusimamisha uso hasa; kwa sababu kuelekea kwa uso kunafuata kuelekea kwa moyo, na hao mawili yanasababisha mwili pia kufanya juhudi. Na ndiyo maana akasema, "kwa unyoofu;" yaani, kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu katika hayo, na kukipa mgongo kila kitu kinginecho. Na jambo hili tulilokuamrisha ndilo "umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu" na akaweka katika akili zao uzuri wake, na akawafanya waone yasiyokuwa hilo kuwa ni mabaya. Kwa maana Mwenyezi Mungu ameweka ndani ya nyoyo za viumbe vyote kuzielekea hukumu zote za kisheria zilizo dhahiri na zilizofichikana, na pia akaweka ndani ya nyoyo zao kupenda haki na kuipendelea. Na huu ndio uhakika wa umbile la asili. Na mwenye kutoka katika msingi huu; basi ni kwa sababu ya jambo lililoingia katika umbile lake la asili na likaliharibu, kama alivyosema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, “Kila mtoto huzaliwa katika umbile la asili. Kisha wazazi wake wanamfanya kuwa Myahudi, au Mkristo, au Majusi.” "Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu." Yaani, hakuna anayeweza kuwabadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu na akawafanya viumbe katika hali nyingine isipokuwa ile ambayo Mwenyezi Mungu aliwaumbia. "Hiyo" ambayo tulikuamrisha "ndiyo Dini iliyonyooka sawa." Yaani, njia iliyonyooka inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na utukufu wake. Kwani, mwenye kuuelekeza uso wake sawasawa kwenye Dini, basi yeye amefuata njia iliyonyooka katika sheria zake zote na njia zake zote, "Lakini watu wengi hawajui" Dini hii iliyonyooka sawa, na hata kama wataijua, hawataifuata.