An-Naml
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
فَتَبَسَّمَ ضَاحِكًا مِّن قَوْلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِىٓ أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ ٱلَّتِىٓ أَنْعَمْتَ عَلَىَّ وَعَلَىٰ وَٰلِدَىَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَـٰلِحًا تَرْضَىٰهُ وَأَدْخِلْنِى بِرَحْمَتِكَ فِى عِبَادِكَ ٱلصَّـٰلِحِينَ ۱۹
{19} Kwa hivyo Suleiman (amani na baraka ziwe juu yake) akaisikia kauli yake na akaielewa, "Basi (Sulaiman) akatabasamu akacheka kwa neno hili" kwa kufurahia ufasaha wake, ushauri wake na usemi wake mzuri. Na hii ndiyo hali ya manabii, rehema na amani ziwe juu yao. Wao wana adabu kamili, na kushangaa katika mahali pake panapostahili, na kwamba hawacheki isipokuwa kutabasamu tu; kama vile Mtume - rehema na amani za mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kilivyokuwa kicheko chake kingi ni kutabasamu tu; kwa maana, kuchekacheka kunaonyesha wepesi wa akili na tabia mbaya. Na kutotabasamu na kustaajabu juu ya mambo ya kushangaza ni katika yale yanayoonyesha tabia mbaya za mtu na kiburi. Na Mitume wametakaswa mbali na hayo. Basi akasema, akimshukuru Mwenyezi Mungu aliyemfikisha katika hali hii: "Ewe Mola wangu Mlezi! Nizindue," na uniwezeshe "niishukuru neema yako uliyonineemesha mimi na wazazi wangu," kwani neema juu ya wazazi ni neema juu ya mtoto. Kwa hivyo akamwomba mola wake mlezi amuwezeshe kushukuru neema yake ya kidini na ya kidunia juu yake na wazazi wake, "na nipate kutenda mema uyapendayo" yenye kuafikiana na amri Yako, yenye kukusudiwa wewe peke yako, yaliyosalimika kutokana na ya kuyaharibu, na kuyapunguza, "na uniingize kwa rehema yako" ambayo miongoni mwake ni Bustani ya mbinguni, "katika waja wako wema" kwani watu wema hupewa rehema kulingana na daraja zao totauti na hadhi zao. Na huu ni mfano ambao Mwenyezi Mungu aliutaja kutoka kwa hali ya Suleiman aliposikia maneno na wito wa mchwa yule.