پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Noor
سورهٔ ۲۴

An-Noor

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۲۶

ٱلْخَبِيثَـٰتُ لِلْخَبِيثِينَ وَٱلْخَبِيثُونَ لِلْخَبِيثَـٰتِ ۖ وَٱلطَّيِّبَـٰتُ لِلطَّيِّبِينَ وَٱلطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَـٰتِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ ۖ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ۲۶

{26} "Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu." Yaani, kila mwovu katika wanaume na wanawake, na maneno na vitendo kinamfaa mtu mbaya, na kuafikiana naye, na kuhusishwa naye, na kufanana naye. Na kila mwema na mzuri katika wanaume na wanawake na maneno na vitendo kinamfaa mtu mbaya, na kuafikiana naye, na kuhusishwa naye, na kufanana naye. Hili ni neno la jumla na lenye mipaka ambalo hakuna kinachoweza kuzuilika kutoka humo. Moja ya maneno yake makubwa zaidi ni kwamba Mitume, hasa wale Ulul-Azm (waliodhamiria zaidi) miongoni mwao, hasa bwana wao Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ambaye ni mbora wa wema miongoni mwa viumbe kwa jumla. Hawawafai hao isipokuwa wanawake. Kumtukana Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwa jambo hili ni kumtukana Mtume -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - na yeye ndiye mkusudiwa wa uzushi huu kutokana na makusudio ya wanafiki. Na kule kuwa kwake tu mke wa Mtume – rehema na amani ziwe juu yake – tayari inajulikana kwamba yeye hawezi kuwa isipokuwa ni mke mwema na msafi kutokana na jambo hili baya. Basi vipi, na yeye si mwingine asipokuwa ni rafiki wa wanawake, mbora wao, mjuzi wao zaidi, kipenzi cha Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote, mke ambaye wahyi haukumteremkia yeye Mtume, huku akiwa katika blanketi na kuliwazwa na mke mwengine asiyekuwa yeye Aisha? Kisha akalibainisha hili kwa namna ambayo haibaki nafasi kwa yeyote aliye mwongo, wala kwa shaka wala dhana yoyote, na akasema, "Hao wameepushwa na hayo wanayoyasema." Na hapa ishara ni kwa Aisha, Mwenyezi Mungu awe radhi naye kwanza, na wanawake waaminifu walio safi na kughafilika, kwa kulingana naye "Msamaha," Utaondoa dhambi. "Na riziki ya ukarimu." Katika Pepo itokayo kwa Mola Mlezi Mkarimu.