پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Taa-Haa
سورهٔ ۲۰

Taa-Haa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۸

ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ ٱلْأَسْمَآءُ ٱلْحُسْنَىٰ ۸

{8} Alipouthibitisha ukamilifu wake kamili katika ujumla wa kuumba kwake na ujumla wa kuamrisha kwake na kukataza kwake, na ujumla wa rehema yake, na upana wa ukuu wake, na kuwa kwake juu ya Kiti chake cha Enzi, na ujumla wa ufalme wake, na ujumla wa elimu yake, ikatokana na hayo kwamba Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa. Na kwamba kumuabudu Yeye tu ndiyo haki inayotakiwa na sheria, akili na maumbile ya asili, na kumwaabudu mwengine ni batili. Akasema, "Mwenyezi Mungu! Hapana mungu yeyote isipokuwa Yeye." Yaani, hakuna muabudiwa wa haki wala mwenye kufanyiwa uungu kwa kuenziwa, udhalilifu, hofu, matumaini, mapenzi, kurudi kwake, na kuombwa dua isipokuwa Yeye. "Yeye ana majina mazuri zaidi," ambayo ni mengi, mazuri, na kamili. Na katika uzuri wake ni kwamba yote ni majina yanayoashiria sifa. Hakuna kati yake jina lolote lisiloashiria sifa na kuhimidiwa. Na katika uzuri wake ni kuwa si nomino za kipekee tu, bali ni nomino za kipekee na sifa. Na katika uzuri wake ni kwamba yanaashiria sifa kamilifu, na kwamba Yeye ndiye Mwenye sifa kamili zaidi katika kila sifa na yenye kujumuisha zaidi na tukufu zaidi. Na katika uzuri wake ni kwamba aliwaamrisha waja wake kwamba wamuombe kwayo, kwa sababu ni njia yenye kumueka mtu karibu naye. Yeye huyapenda na humpenda mwenye kuyapenda, na humpenda mwenye kuyahifadhi, na anampenda anayetafuta kujua maana zake na kumuabudu kwayo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo."