پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۴۴

أَتَأْمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ ٱلْكِتَـٰبَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ۴۴

(44) "Je, mnawaamrisha watu mema" yani imani na heri, wema "na mnazisahau nafsi zenu." Yani mnaziacha bila ya kuziamrisha kufanya hivyo, na hali ni kuwa "nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii." Na akili iliitwa akili kwa sababu anatambua kwayo yale yenye kumnufaisha katika heri, na anajizuia kwayo kutokana na yenye kumdhuru. Na hilo ni kwamba akili inamhimiza aliye nayo kuwa wa kwanza kufanya anachoamrisha, na wa kwanza kuacha anachokataza. Basi mwenye kumwamrisha mwengine kufanya heri; na asifanye yeye, au akamkataza maovu, na asiyaache yeye. Basi hilo linaashiria kutokuwa kwake na akili, na ujinga wake, hasa akiwa analijua hilo, basi hoja imekwishathibiti juu yake. Na aya hii ijapokuwa iliteremka kuhusu Wana wa Israili, ni ya jumla kwa kila mtu kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda?" Na hakuna katika aya hii kuwa ikiwa mtu hafanyi analoamrishwa, aache kuamrisha mema na kukataza maovu. Kwa sababu inaashiria kukemea kuhusiana na haya majukumu mawili, vinginevyo inajulikana kuwa mtu ana kazi mbili: Kuamrisha wengine na kumkataza, na kuiamrisha nafsi yake na kuikataza. Na kuacha moja ya hayo, sio ruhusa ya kuacha hilo lingine. Kwa sababu ukamilifu ni kwamba mwanadamu afanye hizi wajibu mbili. Nao upungufu kamili ni kuyaacha yote mawili. Na ama yeye kufanya moja yake bila ya hilo lingine, siyo katika daraja ya ile hali (kamilifu) ya kwanza, lakini iko kabla ya ile ya mwisho. Na pia, nafsi zimeumbika kutomfuata yule ambaye maneno yake yanapingana na vitendo vyake. Kwa hivyo, kufuata kwao matendo kuko juu zaidi kuliko kuyafuata maneno bure.