Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
ٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مِيثَـٰقِهِۦ وَيَقْطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ ۲۷
Kisha akawaeleza wanaopindukia mipaka, akasema:
(27) “Wanaovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga.” Na hili linajumuisha ahadi iliyopo baina yao na Mola wao Mlezi, na ile iliyopo baina yao na viumbe, ambayo aliisisitiza juu yao kwa maagano mazito na wajibu mbalimbali, kisha hawajali hayo maagano; bali wanayavunja na wanaacha amri zake na wanafanya makatazo yake. Na wanavunja ahadi ambazo zipo baina yao na viumbe wengine. “Na wakayakata aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kuungwa.” Na hili, yanaingia mambo mengi ndani. Kwa maana Mwenyezi Mungu alituamrisha kuunga yaliyopo kati yetu na Yeye, na kumwamini, na kumuabudu. Na yale yaliyopo kati yetu na Mtume wake, kwa kumwamini, na kumpenda, na kumsaidia, na kumtekelezea haki zake. Na yale yaliyopo kati yetu na wazazi wawili, jamaa, marafiki na viumbe wote kwa kuwatekelezea haki zao ambazo Mwenyezi Mungu aliamrisha kwamba tuziunge. Ama Waumini, wao waliunga yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kwamba yaungwe katika haki hizi, na wakayatimiza kikamilifu. Na ama wapotovu, wao waliyakata, na wakayatupa nyuma ya migongo yao, wakayabadilisha na upindukiaji mipaka, na kuyakata na kufanya maasia, nayo ni kufanya uharibifu katika ardhi. Basi “hao” ambao hizi ndizo sifa zao “ndio wenye hasara” katika dunia na Akhera. Na akawa amefungamanisha hasara na wao peke yao. Kwa maana, hasara yao inaingia katika kila hali zao; hawana aina yoyote ya faida. Kwa sababu, kila tendo jema sharti lake ni imani. Naye asiyekuwa na imani, hana matendo. Na hasara hii ndiyo hasara ya ukafiri. Na ama hasara ambayo inaweza kuwa ukafiri na inaweza kuwa maasia, na inaweza kuwa kupuuza kwa kuacha yale yanayopendekezwa, ambayo yametajwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Hakika mwanadamu bila ya shaka yumo katika hasara”, hii ni jumla katika kila kiumbe; isipokuwa mwenye kusifika na imani na matendo mema; na kuusiana kwa haki na kuusiana subira. Na uhakika wake ni kupoteza heri ambayo mja alikuwa karibu mno kuifanya hali ya kuwa ipo katika uwezo wake.