پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
سورهٔ ۲

Al-Baqara

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۲۴

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا۟ وَلَن تَفْعَلُوا۟ فَٱتَّقُوا۟ ٱلنَّارَ ٱلَّتِى وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَـٰفِرِينَ ۲۴

(24) Na aya hii na mfano wake wanaziita Aya za changamoto. Nayo ni kuwashinda viumbe kuleta mfano wa hii Qur-ani au kuipinga kwa namna yoyote. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema "Sema: Wangelikusanyika watu na majini ili walete mfano wa Qur-ani hii, basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao." Hivyo basi, vipi kitaweza kiumbe kilichoumbwa kwa udongo (kusema) kwamba maneno yake ni kama maneno ya Mola Mlezi wa mabwana? Au atawezaje fakiri mwenye upungufu wa namna zote kuleta maneno kama maneno ya yule Mkamilifu ambaye ana ukamilifu wote, na maana pana kwa namna zote? Hili haliko katika uwezekano, wala katika uwezo wa mwanadamu. Na kila mwenye ladha na ujuzi mdogo mno wa aina za maneno, ikiwa ataipima Qur-ani hii [Tukufu] dhidi ya maneno mengineyo ya watu wenye ufasaha, basi tofauti hii kubwa itamdhihirikia. Na katika kauli yake: "Na ikiwa mna shaka" hadi mwisho wake, ipo dalili ya kwamba anayetarajiwa kuongoka kutokana na upotovu ni yule mwenye shaka, aliyechanganyikiwa, ambaye hakuijua haki kutokana na upotovu. Na huyo ndiye yule ambaye akifafanuliwa ukweli, basi atafanya uchu kuufuata ikiwa ni mkweli katika kutafuta haki. Ama mkaidi ambaye anajua haki lakini anaiacha, huyo kurudi kwake hakuwezekani. Kwa sababu, aliiacha haki baada ya kumpambanukia. Hakuiacha kwa ujinga, kwa hivyo hakuna hila katika hilo. Na vile vile mwenye shaka ambaye si mkweli katika kutafuta haki, bali yeye alikengeuka na wala hajitahidi katika kuitafuta; basi na huyu mara nyingi hafanikiwi. Na katika kumuelezea Mtume kuwa ni mja katika huu muktadha mkubwa, kuna dalili ya kwamba sifa yake - rehema na amani ziwe juu yake - kubwa zaidi ni kufanya kwake ibada ambayo hawezi kumfikia katika hilo yeyote miongoni mwa wale wa mwanzo na wa mwisho. Vile vile alimsifu kwa sifa ya uja katika muktadha wa Isra, akasema: "Ametakasika aliyemchukua mja wake usiku"; na katika muktadha wa kuteremsha Ufunuo (wahyi), akasema: "Ni mwenye baraka nyingi aliyeteremsha Al-Furqani (upambanuo) kwa mja wake ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote". Na katika kauli yake "umeandaliwa makafiri" na mfano wake miongoni mwa aya, kuna dalili ya dhehebu la Ahlus-sunna waljama'a kwamba Pepo na Moto vimeshaumbwa, kinyume na Al-Muutazilah. Na ndani yake pia ni kwamba, wanaomwabudu Mwenyezi Mungu peke yake hata wakifanya madhambi makubwa, wao hawatakaa milele Motoni. Kwa sababu alisema, "umeandaliwa makafiri." Na ingekuwa kwamba Waumini wanaofanya maasia watakaa humo milele, basi haungekuwa umeandaliwa makafiri peke yao, tofauti na Al-Khawarij na Al-Mu'utazila. Na ndani yake kuna dalili ya kwamba adhabu inastahiki kutokana na sababu zake, ambazo ni ukafiri, na aina mbalimbali za dhambi.