Al-Baqara
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِى عَنِّى فَإِنِّى قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ ٱلدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا۟ لِى وَلْيُؤْمِنُوا۟ بِى لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ۱۸۶
Hili ni jibu la swali ambalo baadhi ya maswahaba zake walimuuliza Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je, Mola wetu Mlezi yuko karibu, ili tunong’one naye, au yuko mbali ili tumwite kwa sauti kubwa? Basi ikateremka, “na waja wangu watakapokuuliza habari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu.” Kwa sababu yeye Mtukufu ndiye Mwangalizi, Shahidi, mwenye kujua siri na kilichofichika zaidi, anayejua khiyana ya macho na yale ambayo vifua vinaficha. Basi yeye pia yuko karibu na mwenye kumuomba kwa kuitikia, na ndiyo maana akasema: “Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba.” Na dua (kuita) ni aina mbili: Kuita kwa ibada na kuita kwa kuomba jambo. Na ukaribu ni aina mbili: Ukaribu kwa elimu yake juu ya kila kiumbe chake, na ukaribu kwa waja wake na wenye kumuomba kwa kujibu, kusaidia, na kuwezesha. Basi, mwenye kumuomba Mola wake Mlezi kwa moyo uliopo, na dua ya halali, na hakuna kizuizi chochote kinachozuia kuitikia dua hiyo, kama vile kula haramu na mengineyo. Basi Mwenyezi Mungu amemuahidi kumuitikia, na hasa akifanya sababu za kuitikiwa dua. Ambazo ni kumuitikia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kufuata maamrisho yake na kuepuka makatazo yake ya kikauli na kivitendo, na kumuamini, yenye kusababisha aitikiwe. Ndiyo maana akasema: “Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.” Yani watapata kuongoka ambako ndio uwongofu kwenye imani na matendo mema, na wataondolewa upotovu unaopingana na imani na matendo mema. Na kwa sababu kumuamini Mwenyezi Mungu na kuitikia amri yake ni sababu ya kupata elimu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu. “Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu, atakupeni kipambanuzi.” Kisha Mtukufu akasema: