پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Kahf
سورهٔ ۱۸

Al-Kahf

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۵۱

مَّآ أَشْهَدتُّهُمْ خَلْقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَلَا خَلْقَ أَنفُسِهِمْ وَمَا كُنتُ مُتَّخِذَ ٱلْمُضِلِّينَ عَضُدًا ۵۱

{51} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Sikuwafanya mashetani na hawa wapotezao washuhudie uumbaji wa mbingu na ardhi, wala uumbaji wao wenyewe, wala sikutafuta ushauri wao kuhusu hilo. Basi wanawezaje kuwa wao ndio waumbaji wa lolote katika hayo? Bali, aliye wa pekee katika uumbaji, uendeshaji, hekima, kuweka majaliwa ni Mwenyezi Mungu, Muumba wa vitu vyote, aendeshaye mambo yao kwa hekima yake. Basi vipi atafanyiwa washirika miongoni mwa mashetani ili wafanywe vipenzi na kutiiwa jinsi Mwenyezi Mungu anavyotiiwa, na hali hawakuumba, hawakushuhudia uumbaji wowote, na hawakumsaidia Mwenyezi Mungu Mtukufu? Na ndiyo maana akasema, “Wala sikuwafanya wapotoshaji kuwa ni wasaidizi” katika jambo lolote, na wala haimfailii wala haiendani na Mwenyezi Mungu kuwapa sehemu katika uendeshaji. Kwa maana, wanawania kuwapoteza viumbe na kumfanyia uadui Mola wao Mlezi. Basi kinachofaa ziadi ni kuwaweka mbali na wala asiwaweke karibu naye.