Al-Kahf
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسْجُدُوا۟ لِـَٔادَمَ فَسَجَدُوٓا۟ إِلَّآ إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ ٱلْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِۦٓ ۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُۥ وَذُرِّيَّتَهُۥٓ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِى وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّۢ ۚ بِئْسَ لِلظَّـٰلِمِينَ بَدَلًا ۵۰
{50} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu uadui wa Iblisi kwa Adam na kizazi chake. Na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaamuru Malaika wamsujudie Adam kwa heshima, kumtukuza, na kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, basi wakatekeleza hayo, "Isipokuwa Iblisi, yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi" na akasema, "Je, nimsujudie uliyemuumba kwa udongo?" Naye akasema, “Mimi ni bora kuliko yeye.” Kwa hivyo kwa hayo ukabainika uadui wake kwa Mwenyezi Mungu na baba yenu Adam. Basi vipi mnamchukua yeye "na dhuria yake;" yaani, mashetani "kuwa vipenzi badala yangu mimi, na wao ni maadui zenu? Ni ovu mno badala hii ya madhalimu." Yaani, ni ovu mno walilojichagulia wenyewe la kufanya Shetani kuwa kipenzi, ambaye hawaamrishi isipokuwa kufanya mambo machafu na maovu badala ya kumfanya Mwingi wa kurehemu kuwa ndiye kipenzi, ambaye furaha zote na mafanikio yako katika kumfanya yeye kuwa kipenzi. Katika aya hii, kuna himizo la kumfanya Shetani kuwa ni adui na kuwashawishi watu kufanya hivyo, na kutaja sababu ya kulazimu hilo, na kwamba hafanyi yeye kuwa kipenzi isipokuwa dhalimu. Na ni dhuluma gani iliyo kubwa zaidi kuliko dhuluma ya mwenye kumchukua adui yake wa kweli kuwa ndiye kipenzi na kumwacha yule aliye Mlinzi, Msifika? Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi wa wale walioamini. Huwatoa gizani na kuwapeleka kwenye nuru. Lakini wale waliokufuru, walinzi wao ni Mashetani. Huwatoa kwenye nuru na kuwaingiza gizani." Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Hakika wamewafanya mashetani kuwa marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu."