پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Kahf
سورهٔ ۱۸

Al-Kahf

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۴۶

ٱلْمَالُ وَٱلْبَنُونَ زِينَةُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ وَٱلْبَـٰقِيَـٰتُ ٱلصَّـٰلِحَـٰتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ۴۶

{46} Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa fedha mali na watoto ni "pambo la uhai ya dunia" na kwamba hakuna chochote zaidi ya hilo. Na kwamba kile kinachombakia mtu na kumnufaisha na kumfurahisha ni mema yanayobakia. Na hili linajumuisha utiifu wote wa faradhi na ule unaopendekezwa miongoni mwa haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, kama vile swala, zaka, na sadaka na Hajj na Umra, na kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumsifu, na kusema hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kutoa takbira, na kusoma, na kutafuta elimu yenye manufaa, na kuamrisha mema na kukataza maovu, kuwaunga jamaa, kuwafanyia wema wazazi wawili, na kutekeleza haki za mke, watumwa, na mifugo, na mambo yote ya ihsani kwa viumbe. Yote hayo ni miongoni mwa mambo mema yenye kubakia. Haya ndiyo yaliyo bora mbele ya Mwenyezi Mungu kwa malipo, na bora kwa matumaini. Kwa maana, thawabu zake zinabakia na kuongezeka milele, na yanatarajiwa malipo yake, wema wake, manufaa yake yanapohitajika. Basi haya ndiyo washindani wanapaswa kushindania, na watendaji wayakimbilie, na wayafanyie bidii kubwa wafanyao bidii. Na tazama vipi, Mwenyezi Mungu alipopiga mfano wa dunia, hali yake, na kutoweka kwake, akataja kwamba vilivyomo ndani yake ni vya aina mbili: Aina moja ni mapambo yake ambayo watu hujistarehesha kwayo muda kidogo, kisha yanatoweka bila ya manufaa yoyote kumrudia mwenyewe. Na hata labda anaweza kudhuriwa nayo. Haya ni mali na watoto. Na aina ile nyingine ni ya kumbakia mwenyewe milele, ambayo ndiyo mema yenye kubakia.