پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Kahf
سورهٔ ۱۸

Al-Kahf

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۴۵

وَٱضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا كَمَآءٍ أَنزَلْنَـٰهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَٱخْتَلَطَ بِهِۦ نَبَاتُ ٱلْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ ٱلرِّيَـٰحُ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ مُّقْتَدِرًا ۴۵

{45} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - awali na kwa atakayemrithi baada yake pili: Wapigieni watu "mfano wa uhai wa dunia" ili waifikirie ipasavyo na waijue nje na ndani yake, ili wapate kupima kati yake na nyumba inayobakia, na wapendelee ile kati yake inayofailia zaidi kupendelewa. Na kwamba mfano wa uhai wa dunia ni kama mvua inayonyesha juu ya ardhi na ikachanganyika na mimea yake, kisha ikaotesha kila jozi la kupendeza. Na wakati uzuri wake na mapambo yake vilikuwa vinawapendeza watazamaji, na kuwafurahisha wanaofurahia, na kuyavutia macho ya walioghafilika, tazama vikawa "vibuwa vinavyopeperushwa na upepo" kwa hivyo ndipo ikatoweka mimea hiyo ya kupendeza, na uzuri huo mkubwa, na mandhari hayo mazuri. Basi ardhi ikawa vumbi na mchanga ambayo haingaliwi tena, na moyo ukawa mpweke. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo dunia hii, wakati mwenye kuipenda anapokuwa amependezwa na ujana wake, na akawashinda wenzake na rika zake, na akachuma dirhamu na dinari zake, akapata starehe katika mazuri yake, akajiingiza katika matamanio katika wakati wake wote, na akadhani kwamba ataendelea kuwa katika hali hiyo kwa muda siku zake zote zilizobakia, ghafla mauti yakamfika au kuharibika kwa mali yake, kwa hivyo furaha yake hiyo ikatoweka, na raha zake hizo na starehe zikaisha, na moyo wake ukahisi upweke kutokana na maumivu, na ujana wake na nguvu zake na utajiri wake vikaisha, basi akabakia peke yake na matendo yake mema au mabaya. Hapo dhalimu ataing'ata mikono yake atakapojua uhakika wa hali yake na atamani kurejea duniani, si ili akamilishe matamanio yake, bali ili arekebishe yale ambayo aliyapuuza, kwa toba na matendo mema. Basi mwenye akili, mwenye azimio aliyefanikiwa anaiweka hali hii mbele ya nafsi yake, kisha aiambie nafsi yake: Chukulia kwamba umekufa, nawe lazima utakufa. Ni ipi kati ya hali mbili hizi utaichagua: kuhadaika na mapambo ya nyumba hii, ambayo mwenye kujistarehesha kwayo ni kama wanyama walio katika malisho wanavyostarehe. Au aifanyie matendo nyumba ambayo matunda yake ni ya daima, na pia kivuli chake, na ndani yake kuna yale ambayo nafsi zinayatamani na macho yanayafurahia? Basi kwa haya ndiyo inajulikana kuwezeshwa kwa mja au kauchiliwa mbali, na kupata kwake faida au hasara.