پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Israa
سورهٔ ۱۷

Al-Israa

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۱۱

وَقُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُۥ شَرِيكٌ فِى ٱلْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُۥ وَلِىٌّ مِّنَ ٱلذُّلِّ ۖ وَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًۢا ۱۱۱

{111} "Na sema, "Alhamdulillah (sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu)" ambaye ana ukamilifu, na sifa njema, kuhimidiwa, na utukufu kwa namna zote. Naye ametakasika kutokana na kila balaa na kasoro. "Ambaye hakujifanyia mwana yeyote, wala hana mshirika yeyote katika ufalme;" bali ufalme wote ni wa Mwnyezi Mungu, Mmoja, Mshindi. Kwa maana, ulimwengu wa juu na wa chini wote unamilikiwa na Mwenyezi Mungu, na hakuna yeyote aliye na kitu chochote katika umiliki huo, "wala hana mlinzi yeyote wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake." Kwa hivyo, hamfanyi yeyote urafiki katika viumbe vyake ili ajiimarishe naye na ili amsaidie. Kwa maana, Yeye ndiye asiyemhitaji yeyote, Msifika, asiyehitaji chochote katika viumbe wake katika ardhi wala mbinguni, lakini hufanya vipenzi katika viumbe wake ili kuwafanyia wema na kuwarehemu. "Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini. Huwatoa gizani na kuwaingiza katika nuru. "Na mtukuze kwa utukufu mkubwa." Yaani, mfanye ndiye mkuu na umtukuze kwa kujulisha kuhusu sifa zake kubwa, na umsifu kwa majina yake mazuri zaidi, na kwa kumtukuza kwa matendo yake matakatifu, na kwa kumfanya mkuu na kumtukuza kwa kumwabudu Yeye peke yake bila ya mshirika yeyote, na kumfanyia yeye tu dini yote.

Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Isra kupitia mkono wa mwandishi wake Abdur-Rahman bin Nasir bin Abdullah bin Saadi, na kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, na neema na sifa nzuri. Mwenyezi Mungu amsamehe yeye na wazazi wake na waislamu wote. Amin. Na rehema na amani nyingi za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mtume wake Muhammad. Tarehe 7 Jumada Al-Uula, 1344 Hijria. Na niliyatoa haya kutoka katika maandishi ya mwandishi wake kwa kalamu ya maskini kwa Mola wake Mlezi, Suleiman Al-Hamad Al-Bassam, Mwenyezi Mungu amsamehe yeye, wazazi wake na Waislamu wote. Amin. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Muhammad na watu wa familia yake na Maswahaba wake wote. Amin, tena amin.