An-Nahl
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
وَأَلْقَىٰ فِى ٱلْأَرْضِ رَوَٰسِىَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَأَنْهَـٰرًا وَسُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ۱۵ وَعَلَـٰمَـٰتٍ ۚ وَبِٱلنَّجْمِ هُمْ يَهْتَدُونَ ۱۶
{15 - 16} Yaani, "Na akaweka" Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waja wake "katika ardhi milima madhubuti" ili isiyumbe yumbe nao ana kuwasumbua viumbe, ndiyo waweze kulima ardhi, na kujenga, na kutembea juu yake. Na katika rehema yake Yeye Mtukufu aliweka humo mito anayoiendesha kutoka ardhi ya mbali hadi ardhi ambayo inaihitaji kwa lazima katika kunywa kwao na kunywesha mifugo wao na mashamba yao. Kuna mito ya juu ya uso wa ardhi na mingine ndani ya ardhi ambayo wanaitoa nje kwa kuchimba mpaka waifikie kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu amewatiishia miongoni mwa ndoo za kutekea, na ala mbalimbali na mfano wake. Na katika rehema zake ni kwamba alifanya katika njia mbalimbali za kufikisha katika miji ya mbali "ili mpate kuongoka" katika njia hizo, kiasi kwamba unaweza kupata ardhi iliyoshikamana kwa milima inayofuatana lakini Mwenyezi Mungu ameweka kati yake mapitio kwa wapitao.