Hud
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِۦ وَيَتْلُوهُ شَاهِدٌ مِّنْهُ وَمِن قَبْلِهِۦ كِتَـٰبُ مُوسَىٰٓ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِۦ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِهِۦ مِنَ ٱلْأَحْزَابِ فَٱلنَّارُ مَوْعِدُهُۥ ۚ فَلَا تَكُ فِى مِرْيَةٍ مِّنْهُ ۚ إِنَّهُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ ۱۷
{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaitaja hali ya Mtume wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - na wale walioshika nafasi yake katika warithi wake ambao wanaisimamisha dini yake, na hoja zake, wale ambao wana yakini na hayo. Na kwamba, hakuna yeyote anayeweza kusifiwa kwa sifa zao na kwamba mtu yeyote hawezi kuwa mfano wao. Akasema, "Basi je, yule ambaye ana ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wake Mlezi" kwa wahyi aliouteremsha Mwenyezi Mungu ukiwa ndani yake na masuala muhimu na ushahidi wake ulio dhahiri, basi akawa na yakini na ushahidi huo ulio wazi, "na unaofuatwa." Yaani, ushahidi huu na hoja hii vikafuatwa na uthibitisho mwingine, ambao ni "na shahidi anayetoka kwake." Naye ni shahidi wa maumbile ya asili yaliyonyooka, na akili timamu, aliposhuhudia kwa uhakika yale aliyoyafunua Mwenyezi Mungu na sheria yake, na akajua kwa akili yake uzuri wake, kwa hivyo akazidi kwa sababu ya hilo imani juu ya imani "na" kisha kuna shahidi wa tatu. Nayo ni "Kitabu cha Musa," Taurati ambayo Mwenyezi Mungu aliifanya kuwa "mwongozi" kwa watu "na rehema" kikiishuhudilia Qur-ani hii kuwa ni ukweli na inaafikiana nayo katika yale iliyokuja nayo ya haki. Yaani, Je, kuna mtu mwenye sifa hizi, ambaye amekuwa akijiwa na ushahidi wa imani na hoja za yakini zikamsimamia, je yeye ni kama yule ambaye yuko katika giza mbalimbali na ujinga mwingi ambavyo hawezi kutoka nje yake? Hawawi sawa kwa Mwenyezi Mungu wala kwa waja wa Mwenyezi Mungu. "Hao;" Yaani, wale ambao waliwezeshwa kusimamiwa na ushahidi, hao wanaiamini Qur’ani kwa uhakika, kwa hivyo imani yao hiyo ikawasababishia heri katika dunia hii na Akhera. "Naye anayeikufuru" yaani, Qur’ani, "katika makundi." Yaani, makundi mengineyo yote ya watu wa ardhi wanaofanya makundi ya kuikataa haki, "basi Moto ndipo pahali pa miadi yake" ni lazima atauingia. "Kwa hivyo, usiwe katika shaka [juu yake]" yaani, hata shaka kidogo tu. "Hakika, hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi, lakini wengi wa watu hawaamini." Ima kwa ujinga wao tu na upotofu, na ima kwa dhuluma, ukaidi, na kuvuka mipaka. Na kama sivyo, mwenye makusudio mazuri na ufahamu wake umenyooka, basi ni lazima aiamini; kwa sababu, anaona kile kinachomwita kwenye imani kutoka kila pembe.