پرش به محتوا
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yunus
سورهٔ ۱۰

Yunus

این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همان‌گونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر می‌کند و از صفحه‌های آن سایت گرفته شده است. سایت نمی‌گوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی می‌کند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمی‌کند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیه‌هایی آمده که دربارهٔ آن‌ها توضیح می‌دهد و این آیه‌ها متن قرآن از Tanzil است، همان‌گونه که آنجا هست؛ آیه‌ای که سایت توضیح جداگانه‌ای برایش نمی‌دهد با بخش پیش از خود می‌آید، و فهرست هر چنین آیه‌ای را نام می‌برد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.

متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشته‌شده در 2026-10-22

آیهٔ ۱۰۷

وَإِن يَمْسَسْكَ ٱللَّهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُۥٓ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَآدَّ لِفَضْلِهِۦ ۚ يُصِيبُ بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ ۚ وَهُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ ۱۰۷

{107} Huu ni katika ushahidi mkubwa zaidi kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa. Kwani yeye tu ndiye mwenye kunufaisha, mwenye kudhuru, mwenye kupeana, mwenye kunyima, ambaye anapogusa kwa madhara kama vile umaskini, na maradhi na mengineyo, "basi hakuna wa kukuondolea isipokuwa Yeye" kwa sababu lau kuwa viumbe vingekusanyika ili kunufaisha kwa kitu fulani, basi havingenufaisha isipokuwa tu kwa kile alichokiandika Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa wangekusanyika ili kumdhuru yeyote, basi Hawangeweza chochote katika kumdhuru ikiwa [Mwenyezi Mungu] hakutaka hilo. Na ndio maana akasema: "Na akikutakia heri, basi hakuna wa kurudisha fadhila yake" Yaani hawezi yeyote miongoni mwa viumbe kurudisha fadhila yake na wema wake, kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu, basi hakuna wa kuizuia. Na anayoizuia, hakuna wa kuiachilia isipokuwa Yeye." "Humsibu kwayo amtakaye katika waja wake" yaani humchagua kumpa rehema zake amtakaye miongoni mwa viumbe vyake, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa. {Na Yeye ni Mwenye kusamehe" makosa yote, ambaye humuwezesha mja wake kufikia sababu za maghufira, kisha mja anapozifanya, Mwenyezi Mungu humsamehe madhambi yake yote, makubwa yake na madogo yake. {Mwenye kurehemu} ambaye rehema yake imeenea kwa kila kitu, na ukarimu wake ulikifikia kila kitu kilichopo kwa namna kwamba hawawezi kujitosheleza bila ya wema wake kwa muda wa kupepesa jicho. Basi mja anapojua kwa ushahidi wa kukata kwamba Mwenyezi Mungu ndiye peke yake mwenye kuneemesha, na kuondoa adhabu, na kupeana mazuri, na kuondoa mabaya na balaa, na kwamba hakuna yeyote miongoni mwa viumbe aliye na chochote katika haya mkononi mwake isipokuwa yale aliyoyafanyisha Mwenyezi Mungu kupitia mikononi mwake. Basi atakuwa na yakini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa haki, na ya kwamba wale wanaowaomba badala yake ndio wa batili, na ndiyo maana alipobainisha ushahidi ulio wazi, akasema baada yake: