An-Nisaa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَمَا لَكُمْ لَا تُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلْوِلْدَٰنِ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَخْرِجْنَا مِنْ هَـٰذِهِ ٱلْقَرْيَةِ ٱلظَّالِمِ أَهْلُهَا وَٱجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَٱجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا 75
{75} Huku ni kuhimiza kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake Waumini, na kuamsha hisia zao juu ya kupigana vita katika njia yake, na kwamba hilo limeshawalazimu wao na lawama kubwa imewaelekea kwa kuiacha. Kwa hivyo, akasema, “Na mna nini hampigani katika Njia ya Mwenyezi Mungu” na hali ni kwamba wanaoonewa miongoni mwa wanaume, na wanawake, na watoto ambao hawawezi kufanya hila wala hawawezi kufuata njia sawasawa. Na pamoja na haya, walikwisha patwa na dhuluma kubwa zaidi kutoka kwa maadui zao. Kwa hivyo, wao wanamwomba Mwenyezi Mungu kwamba awatoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu juu ya nafsi zao kwa ukafiri na ushirikina, na kwa kuwadhuru Waumini na kuwazuia njia ya Mwenyezi Mungu, na kuwazuia kuilingania dini yao na kuhama. Na wanamwomba Mwenyezi Mungu kwamba awafanyie mlinzi na msaidizi atakayewaokoa kutoka katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu. Kwa hivyo, yakawa mapambano yao kwa namna hii ni katika mlango wa kupigana vita, na kuzilinda familia zao, na watoto wao, na jamaa zao. Kwa sababu, mlango wa jihadi ambao ni kutaka kupambana na makafiri, hata kama una fadhila kubwa ndani yake, na mwenye kubaki nyuma yake analaumiwa kwa hilo lawama kubwa. Lakini Jihadi ambayo ndani yake kuna kuwaokoa wanaoonewa miongoni mwenu ina malipo makubwa zaidi na manufaa makubwa zaidi, kwani ni katika mlango wa kuwazuia maadui.