Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sūrah 4

An-Nisaa

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 7

لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ ٱلْوَٰلِدَانِ وَٱلْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَآءِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ ٱلْوَٰلِدَانِ وَٱلْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ ۚ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا 7

{7} Waarabu wakati wa Jahiliyya kwa sababu ya ukatili wao na ugumu wao walikuwa hawawarithishi wanyonge kama vile wanawake na watoto. Na walikuwa wakiwagawia urithi wanaume wenye nguvu tu. Kwa sababu walikuwa wakidai kuwa wao tu ndio wanaoweza vita, na kupigana, na kunyang’anya, na kupora. Kwa hivyo, Yeye Mola Mlezi, Mwenye rehema, Mwenye hekima akataka kuwawekea waja wake sheria ambayo wako sawa wanaume wao na wanawake wao, wenye nguvu wao na wanyonge wao. Na aliweka mbele ya hayo jambo la jumla ili nafsi zilizoee hilo, kisha maelezo ya kina yaje baada ya ujumla ambao nafsi zina shauku juu yake, na kuondoka kwa unyama ambao unatokana na ada mbaya. Na akasema, “Wanaume wana fungu,” yani, sehemu; “katika yale wanayoyaacha wazazi;” yani, baba na mama, “na jamaa wa karibu.” Na huu ni ujumla baada ya umahususi. “Na wanawake wanalo fungu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa wa karibu.” Basi ni kana kwamba ilisemwa: Je, fungu hilo linarejea kwa desturi na ada na kwamba wawape wanachotaka au ni kitu kilichopimwa? Kwa hivyo, Yeye Mtukufu akasema, “Ni mafungu yaliyofaradhiwa.” Yani, ameshayapima Yeye Mwenye kujua, Mwenye hekima. Na Mwenyezi Mungu akipenda, utakuja ubaninisho wa hilo. Na pia, hapa kuna fikira nyingine potofu: pengine mtu anaweza kufirikia kwamba wanawake na watoto hawana fungu isipokuwa katika mali nyingi. Kwa hivyo, akaondoa hilo kwa kauli yake, “Kwa kile kilicho kidogo chake au kingi.” Basi ni Mwenye baraka nyingi Yeye ambaye ndiye mbora wa wanaohukumu.