Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sūrah 2

Al-Baqara

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 38

قُلْنَا ٱهْبِطُوا۟ مِنْهَا جَمِيعًا ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّى هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَاىَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ 38

(38) Alirudia kuteremka, ili yapatikane yale yaliyotajwa, nayo ni kauli yake “na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu.” Yani wakati utakapowajia kutoka kwangu - Enyi kundi la wazito wawili - uwongofu, yani Mtume na Kitabu kinachowaongoza kwenye yale yenye kuwaweka karibu na Mimi, na yenye kuwaweka karibu na radhi zangu. Basi watakaofuata uwongofu wangu huo miongoni mwenu, kwa kuwaamini Mitume wangu na Vitabu vyangu, na akaongoka nao. Na hilo ni kwa kusadiki habari zote za Mitume na Vitabu, na kutekeleza amri, na kujiepusha na makatazo. “Basi haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.” Na katika aya nyingine “basi atakayeufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.” Kwa hivyo, akafungamanisha mambo manne na kufuata mwongozo wake: Kukanusha hofu na huzuni. Na tofauti iliyopo kati ya hayo ni kuwa chenye kuchukiza ikiwa kilikuwa kimeshapita, huwa kinaleta huzuni. Na ikiwa bado kinangonjewa, huwa kinaleta hofu. Basi akayakanusha haya mawili kwa mwenye kufuata uwongofu wake. Na mawili haya yasipokuwa, basi kinyume chake kinatokea, nacho ni amani kamili.