Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَلَا تَجْعَلُوا۟ ٱللَّهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَـٰنِكُمْ أَن تَبَرُّوا۟ وَتَتَّقُوا۟ وَتُصْلِحُوا۟ بَيْنَ ٱلنَّاسِ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ 224
{224} Maana ya kiapo, ni kumtukuza yule ambaye imeapwa kwa jina lake, na kusisitiza kilichoapwa kutekelezwa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alikuwa ameamrisha kuhifadhi viapo. Na hilo lilikuwa linahitaji vihifadhiwe katika kila kitu. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alitoa katika hali hiyo inapokuwa kutekeleza kiapo kunajumuisha kuacha yale ambayo ni wajibu zaidi kwake. Kwa hivyo, akawakataza waja wake kuvifanya viapo vyao kuwa kisingizio, yani kipingamizi na kizuizi cha wao kufanya wema: Kama kufanya wema, au kuepuka shari (uovu), au kupatanisha baina ya watu. Basi anayeapa kuacha wajibu, italazimu ivunjwe, na ni haramu kuendelea kukishikilia kiapo chake hicho. Na mwenye kuapa kuacha kitu kinachopendekezwa, itapendekezwa kwamba aivunje. Na mwenye kuapa kufanya jambo la haramu, italazimu ivunjwe. Na ama jambo linaloruhusika, hilo inafaa kukihifadhi kiapo kisivunjwe. Aya hii inatumika kama ushahidi juu ya misingi maalumu wa kwamba, “ikiwa masilahi yataingiliana, basi litapewa kipaumbele lililo muhimu zaidi kati yake.” Na hapa, kutimiza kiapo ni masilahi, na kutii amri za Mwenyezi Mungu katika mambo haya ni masilahi makubwa kuliko hilo. Kwa hivyo, hili likapewa kipaumbele kwa sababu ya hilo. Kisha akahitimisha Aya hii kwa majina haya mawili matukufu, akasema, “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia” yani sauti zote “Mwenye kujua” wa makusudio na nia. Na katika hayo, ni kusikia kwake maneno ya wanaoapa, na kujua kwake, makusudio yao. Je, ni heri au shari (maovu)? Na ndani ya hilo kuna onyo dhidi ya malipo yake, na kwamba matendo yenu na nia zenu, tayari elimu ya hayo imeshatulia kwaye.