Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا۟ حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا۟ لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُم مُّلَـٰقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ 223
(223) “Wake zenu ni konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo” kwa kutokea mbele na kwa kutokea nyuma. Lakini isiwe isipokuwa katika uke, kwa sababu ndipo pahali pa kulima, na ndipo pahali ambapo mtoto hutokana napo. Na kuna ushahidi wa kuharamishwa kujamiiana kwenye tupu ya nyuma. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu hakuruhusu kumuingilia mwanamke isipokuwa katika mahali ambapo kuna kulima. Na kuna hadithi nyingi za Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika kuharamisha hilo, na kumlaani mwenye kulifanya. “Lakini zitangulizieni heri nafsi zenu.” Yani kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kutenda mema. Na katika hayo ni mtu kumpapasa mkewe na kumuingilia kwa namna ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kutaraji malipo, na kwa kutaraji kupata kizazi ambacho Mwenyezi Mungu atafaidisha kwao. “Na mcheni Mwenyezi Mungu” yani katika hali zenu zote. Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, mkitafuta msaada katika hilo, mkijua, “hakika nyinyi mtakutana naye.” Na atawalipa kwa matendo yenu mema na mengineyo. Kisha akasema: “Na wape habari njema Waumini,” lakini hakutaja ni bishara njema ya nini ili iashirie ujumla. Na kwamba wana bishara njema katika maisha ya duniani na katika Akhera. Na kila kheri, na kuepushwa na kila shari vinavyofungamanishwa na imani, basi inaingia katika bishara njema hii. Na ndani yake kuna mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa Waumini, na mapenzi ya yale yanayowafurahisha, na kupendekeza kuwasisimua na kuwatia shauku kwa yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu ya malipo ya kidunia na ya kiakhera.