Al-Maaida
এটি আস-সা‘দীর তাফসীরের একটি অনুবাদ, IslamHouse.com যেভাবে saadi.islamenc.com-এ প্রকাশ করে, সেই সাইটের পাতা থেকে পড়া। সাইটটি বলে না কে এটি অনুবাদ করেছেন বা এটি ছাপা কোন সংস্করণ অনুসরণ করে, এবং এর পাঠ নেওয়ার কোনো শর্তও জানায় না, তাই এটি দেখানোর অধিকার যাচাই করা হয়নি। কেউ এটিকে ছাপা বইয়ের সঙ্গে মেলায়নি এবং কোনো আলেম এটি পর্যালোচনা করেননি। প্রতিটি অংশ যে আয়াতগুলোর উপর মন্তব্য করে তার পাশে আছে; আয়াতগুলো Tanzil-এর কুরআনের পাঠ, সেখানে যেমন আছে তেমন দেখানো; যে আয়াতের জন্য সাইটটি আলাদা কোনো ব্যাখ্যা দেয় না, সেটি তার আগের অংশের সঙ্গে থাকে, আর সূচি এমন প্রতিটি আয়াতের নাম করে। সাবীল এর কিছুই লেখেনি বা অনুবাদ করেনি।
পাঠ নেওয়া হয়েছেsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22-এ নেওয়া
وَأَنِ ٱحْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَآءَهُمْ وَٱحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَنۢ بَعْضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيْكَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَٱعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلنَّاسِ لَفَـٰسِقُونَ ৪৯
{49} "Na hukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu." Aya hii ndiyo iliyosemwa inafuta kauli yake: "Basi hukumu baina yao au wapuuze." Na mtazamo sahihi ni kuwa haikubatilishwa, na kwamba Aya ile inaashiria kwamba yeye - Swalah ya Mwenyezi Mungu na amani ziwe juu yake, - ana hiari baina ya hukumu kati yao au kutofanya hivyo. Na hilo ni kwa sababu hawakuikusudia haki. Nayo Aya hii inaashiria kwamba ikiwa atahukumu, basi ahukumu kati yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu na Sunnah. Nao ni uadilifu ambao ulitangulia kuwa Mwenyezi Mungu alisema; "Na ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu." Na hili liliashiria kubainisha uadilifu, na kwamba kiini chake ni hukumu alizoziweka Mwenyezi Mungu. Kwani zinajumuisha uadilifu wa juu zaidi na haki, na kila lililo kinyume na hilo ni ukandamizaji na dhulma. "Wala usifuate matamanio yao." Alirudia katazo la kufuata matamanio yao kwa sababu ya ukali wa onyo dhidi yake, na kwa sababu ile ni katika nafasi ya kuhukumu na kutoa fatwa, ambayo ni pana zaidi. Na hii ni katika nafasi ya kuhukumu peke yake, na katika yote mawili ni wajibu kwake kutofuata matamanio yao yanayohalifiana na haki. Na ndiyo maana akasema, "Na watahadhari wasije wakakufitini ukaacha baadhi ya yale aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu." Yaani, jihadhari na kudanganywa nao, na kufitinishwa nao wakakuzuia baadhi ya yale aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo kukawa kufuata matamanio yao ndiyo sababu inayopelekea kuacha haki ya wajibu, na makusudio ni kuifuata. "Na wakigeuka," wakaacha kukufuata wewe na kuacha kufuata haki, "basi jua kwamba" hiyo ni adhabu, na kwamba Mwenyezi Mungu anataka awasibu kwa baadhi ya madhambi yao. Kwani madhambi yana adhabu za sasa na za baadaye. Na miongoni mwa adhabu kubwa zaidi ni kuwa mja ajaribiwe na apambiwe kuacha kumfuata Mtume, na hilo ni kwa sababu ya kupita kwake mipaka. "Na hakika wengi miongoni mwa watu ni wenye kupita mipaka." Yaani, maumbile yao ni kupita mipaka na kutoka katika kumtii Mwenyezi Mungu na kumfuata Mtume wake.