মূল অংশে যান
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
সূরা ৫

Al-Maaida

এটি আস-সা‘দীর তাফসীরের একটি অনুবাদ, IslamHouse.com যেভাবে saadi.islamenc.com-এ প্রকাশ করে, সেই সাইটের পাতা থেকে পড়া। সাইটটি বলে না কে এটি অনুবাদ করেছেন বা এটি ছাপা কোন সংস্করণ অনুসরণ করে, এবং এর পাঠ নেওয়ার কোনো শর্তও জানায় না, তাই এটি দেখানোর অধিকার যাচাই করা হয়নি। কেউ এটিকে ছাপা বইয়ের সঙ্গে মেলায়নি এবং কোনো আলেম এটি পর্যালোচনা করেননি। প্রতিটি অংশ যে আয়াতগুলোর উপর মন্তব্য করে তার পাশে আছে; আয়াতগুলো Tanzil-এর কুরআনের পাঠ, সেখানে যেমন আছে তেমন দেখানো; যে আয়াতের জন্য সাইটটি আলাদা কোনো ব্যাখ্যা দেয় না, সেটি তার আগের অংশের সঙ্গে থাকে, আর সূচি এমন প্রতিটি আয়াতের নাম করে। সাবীল এর কিছুই লেখেনি বা অনুবাদ করেনি।

পাঠ নেওয়া হয়েছেsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22-এ নেওয়া

আয়াত ৪

يَسْـَٔلُونَكَ مَاذَآ أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ ٱلطَّيِّبَـٰتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ ٱلْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ ٱللَّهُ ۖ فَكُلُوا۟ مِمَّآ أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَٱذْكُرُوا۟ ٱسْمَ ٱللَّهِ عَلَيْهِ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ ৪

{4} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad -rehema na amani zimshukie, - "Wanakuuliza ni nini wamehalalishiwa?" Miongoni mwa vyakula. "Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri," navyo ni kila chenye manufaa au raha bila ya kuudhuru mwili wala akili. Kwa hivyo ikaingia katika hilo nafaka zote na matunda ambavyo viko katika vijiji na mashamba, na wakaingia katika hilo wanyama wote wa baharini na wanyama wote wa nchi kavu. Isipokuwa wale waliotolewa katika hilo na Sheria, kama vile wanyama-mwitu na wanyama wachafu miongoni mwao. Ndiyo maana iliashiria Aya hii kwa maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja kwamba mambo machafu yameharamishwa. Kama ilivyosemwa hilo waziwazi katika kauli yake Yeye Mtukufu, "na anawahalalishia vilivyo vizuri, na anawaharimishia viovu. "Na mlichowafundisha wanyama kukiwinda." Yaani mmehalalishiwa mlichowafunza katika wanyama wa kuwinda... mpaka mwisho wa Aya. Aya hii iliashiria mambo mbalimbali: Moja yake ni upole wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake na rehema yake juu yao, kwa kuwa amewapanulia njia za halali, na akawaruhusu kile ambacho hawakuchinja miongoni mwa vile ambavyo viliwindwa na wanyama wa kuwindia. Na maana ya wanyama wa kuwindia ni mbwa, simbamarara, na kipanga, na mfano wa hao miongoni mwa wale wanaowinda kwa meno yake na kucha zake. La pili ni sharti kwamba awe amefundishwa kwa kile kinachochukuliwa kulingana na ada kwamba amefundishwa, kama vile aende anapoambiwa kwenda, na akomeke anapoambiwa kukoma, na anapokamata, hamli. Na kwa sababu ya hiyo ndiyo akasema, "Mnawafundisha alivyowafunzeni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni katika kile walichowakamatia." Yaani, waliwakamata mawindo kwa ajili yenu. Na kile alichokula kwacho mnyama wa kuwinda, haijulikani ikiwa alimuwinda kwa ajili ya mwenyewe, na huenda alimuwinda kwa ajili ya nafsi yake. La tatu: Ni sharti kwamba mbwa au ndege au mfano wake wamjeruhi kwa sababu ya kauli yake "wanyama kukiwinda," pamoja na uharamu uliotangulia kuhusiana na yule aliyenyongwa. Basi ikiwa mbwa au mwingine au alimuua kwa uzito wake, basi hili haliruhusiwi, kwa kuzingatia kwamba al-jawarih ni wale wenye kuwajeruhi mawindo kwa meno yao na kucha zao. Lakini maana mashuhuri ni kuwa al-jawarih ni wale wenye kumtafuta na kumkamata windo. Na kwa maana hii, hilo la kujeruhi haliwi sharti. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi. La nne ni kuruhusika kwa kummiliki mbwa wa kuwinda. Kama ilivyokuja katika hadithi sahihi, pamoja na kwamba kummiliki mbwa ni haramu. Kwa sababu yanayoambatana na uhalali wa windo lake na kumfundisha mbwa kwake, ni kuruhusika kummiliki. La tano ni usafi wa kile kilichoguswa na mdomo wa mbwa katika windo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliiruhusu na hakutaja kumuosha kokote, kwa hivyo hilo likaashiria usafi wake. La sita ni kwamba ndani yake kuna ubora wa elimu. Na kwamba mnyama wa kuwindia kwa sababu ya elimu ndiyo kikaruhusika kile alichowinda, ilhali asiyejua mfundisho, huyo windo lake haliruhusiwi. La saba ni kwamba kujishughulisha na kumfundisha mbwa au ndege au wengineo si jambo la kulaumiwa juu yake, na si jambo la kipuuzi na batili. Bali ni jambo linalokusudiwa. Kwa sababu ni njia ya kuhalalisha windo lake na kufaidika kwaye. La nane ni kwamba ndani yake kuna hoja ya aliyeruhusu kumuuza mbwa wa kuwinda. Alisema: Kwa sababu huenda hawezi kumpata isipokuwa kwa hilo. La tisa ni kwamba ndani yake kuna sharti la kumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kumwachilia mnyama wa kuwinda, na kwamba ikiwa hatamtaja Mwenyezi Mungu kwa maksudi, basi hangeruhusiwa kile kilichouawa na huyo mnyama wa kuwinda. La kumi ni kwamba inaruhusika kula kile kilichokamatwa na mnyama wa kuwinda, sawa awe alimuua au hapana. Na kwamba ikiwa mmiliki wake atamkuta hali ya kuwa kuna uhai mtulivu ndani yake, basi haruhusiwi isipokuwa kwa hilo. Kisha Yeye Mtukufu akahimiza juu ya kumcha Yeye na akatahadharisha juu ya kuijia hesabu katika Siku ya Qiyama. Na kwamba hilo ni lililokwisha karibia, kwa hivyo akasema, "Na mcheni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu."