মূল অংশে যান
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
সূরা ২

Al-Baqara

এটি আস-সা‘দীর তাফসীরের একটি অনুবাদ, IslamHouse.com যেভাবে saadi.islamenc.com-এ প্রকাশ করে, সেই সাইটের পাতা থেকে পড়া। সাইটটি বলে না কে এটি অনুবাদ করেছেন বা এটি ছাপা কোন সংস্করণ অনুসরণ করে, এবং এর পাঠ নেওয়ার কোনো শর্তও জানায় না, তাই এটি দেখানোর অধিকার যাচাই করা হয়নি। কেউ এটিকে ছাপা বইয়ের সঙ্গে মেলায়নি এবং কোনো আলেম এটি পর্যালোচনা করেননি। প্রতিটি অংশ যে আয়াতগুলোর উপর মন্তব্য করে তার পাশে আছে; আয়াতগুলো Tanzil-এর কুরআনের পাঠ, সেখানে যেমন আছে তেমন দেখানো; যে আয়াতের জন্য সাইটটি আলাদা কোনো ব্যাখ্যা দেয় না, সেটি তার আগের অংশের সঙ্গে থাকে, আর সূচি এমন প্রতিটি আয়াতের নাম করে। সাবীল এর কিছুই লেখেনি বা অনুবাদ করেনি।

পাঠ নেওয়া হয়েছেsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22-এ নেওয়া

আয়াত ২৬

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسْتَحْىِۦٓ أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَيَقُولُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِۦ كَثِيرًا وَيَهْدِى بِهِۦ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِۦٓ إِلَّا ٱلْفَـٰسِقِينَ ২৬

(26) Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema “Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano.” Yani mfano wowote ule “wa mbu na ulio wa zaidi yake.” Kwa sababu mifano ina hekima, na kubainisha ukweli, na Mwenyezi Mungu haoni haya juu ya haki. Na ni kana kwamba katika hili kuna jibu kwa wale waliopinga kupiga mfano katika vitu duni, na wakampinga Mwenyezi Mungu katika hilo. Lakini hakuna upingamizi wowote katika hilo. Bali ni mafundisho ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na rehema yake juu yao. Basi ni lazima ipokewe (mifano hiyo) kwa kuikubali na kushukuru. Ndio maana akasema: “Ama wale walioamini hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi,“ wao wanatafuta kuifahamu na wanaitafakari. Hivyo, wakijua kilichomo ndani yake kwa undani, basi elimu yao na imani yao vinaongezeka. Vinginevyo, wanajua kwamba ni kweli, na kile kilichomo ni kweli, hata ikiwa namna wa ukweli humo ndani yake itafichika kwao. Kwa sababu wajua kwamba Mwenyezi Mungu hakuipiga (mifano hiyo) bure, bali kwa hekima kubwa na neema nyingi. “Lakini wale waliokufuru husema: Ni nini analokusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu?” Basi wao wanapinga na wanatahayari, hivyo wanazidisha ukafiri juu ya ukafiri wao, kama vile Waumini walivyozidisha imani juu ya imani yao. Ndio maana alisema “Kwa mfano huu huwapoteza wengi na huwaongoa wengi.” Na hii ndiyo hali ya Waumini na makafiri wakati wa kuteremka kwa aya za Qur-ani. Mwenyezi Mungu amesema: “Na inapoteremshwa Sura wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Ama wale walioamini inawazidishia Imani, nao wanafurahi. Ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi inawazidishia uovu juu ya uovu wao; na wanakufa hali ni makafiri.“ Kwa hivyo, hakuna neema kubwa kwa waja kuliko kuteremka kwa aya za Qur-ani. Na pamoja na hayo zinakuwa kwa watu wengine mtihani na tahayari, na upotovu, na kuongezeka kwa uovu juu ya uovu wao. Na kwa watu wengine ni hiba na rehema na kuzidishiwa heri juu ya heri yao. Basi ametakasika yule aliyetofautisha kati ya waja wake, na akapwekeka katika kuongoza na kupoteza. Kisha akataja hekima yake na uadilifu wake katika kuwapoteza yeye wale anaowapoteza, akasema: “Lakini hawapotezi ila wale wanaopindukia mipaka.” Yani wale wanaotoka katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu, wanaowapinga Mitume wa Mwenyezi Mungu, ambao hupindukia mipaka imekuwa sifa yao, hivyo hawatafuti badala ya hilo. Kwa hivyo, hekima yake Mtukufu ikahitaji wapotezwe, kwa sababu hawakuufalia uongofu, kama ilivyohitaji hekima yake na neema yake kumwongoza yule ambaye anasifika kwa sifa ya imani na akajipamba kwa matendo mema. Na kupindukia mipaka ni aina mbili: Aina ya kumtoa mtu katika dini. Nako ni kupindukia mipaka kunakomlazimu (mtu) kutoka katika imani; kama kule kulikotajwa katika aya hii na mfano wake. Na aina nyingine siyo ya kumtoa mtu katika imani, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Enyi mlioamini, akikujieni mpotofu na habari yoyote, chunguzeni...” hadi mwisho wa aya.