মূল অংশে যান
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
সূরা ২

Al-Baqara

এটি আস-সা‘দীর তাফসীরের একটি অনুবাদ, IslamHouse.com যেভাবে saadi.islamenc.com-এ প্রকাশ করে, সেই সাইটের পাতা থেকে পড়া। সাইটটি বলে না কে এটি অনুবাদ করেছেন বা এটি ছাপা কোন সংস্করণ অনুসরণ করে, এবং এর পাঠ নেওয়ার কোনো শর্তও জানায় না, তাই এটি দেখানোর অধিকার যাচাই করা হয়নি। কেউ এটিকে ছাপা বইয়ের সঙ্গে মেলায়নি এবং কোনো আলেম এটি পর্যালোচনা করেননি। প্রতিটি অংশ যে আয়াতগুলোর উপর মন্তব্য করে তার পাশে আছে; আয়াতগুলো Tanzil-এর কুরআনের পাঠ, সেখানে যেমন আছে তেমন দেখানো; যে আয়াতের জন্য সাইটটি আলাদা কোনো ব্যাখ্যা দেয় না, সেটি তার আগের অংশের সঙ্গে থাকে, আর সূচি এমন প্রতিটি আয়াতের নাম করে। সাবীল এর কিছুই লেখেনি বা অনুবাদ করেনি।

পাঠ নেওয়া হয়েছেsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22-এ নেওয়া

আয়াত ২১৫

يَسْـَٔلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ ۖ قُلْ مَآ أَنفَقْتُم مِّنْ خَيْرٍ فَلِلْوَٰلِدَيْنِ وَٱلْأَقْرَبِينَ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينِ وَٱبْنِ ٱلسَّبِيلِ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٌ ২১৫

{215} Yani wanakuuliza juu ya kutoa matumizi. Na hili linajumuisha kuuliza kuhusu mtoaji na anayepewa. Basi akawajibu hayo, akasema. “Sema: Chochote mnachotoa katika heri,” yani mali kidogo au nyingi, basi watu wanaoistahili zaidi, na wanaostahiki zaidi kutangulizwa, ni wale wenye haki kubwa zaidi juu yako. Nao ni wazazi wawili ambao ni wajibu kuwafanyia wema, ambao ni haramu kuwa na utovu na nidhamu kwao na kuacha kuwapa matumizi. Ndiyo maana kuwapa matumizi ni wajibu juu ya mtoto mwenye wasaa. Kisha baada ya wazazi ni jamaa wa karibu zaidi kulingana na tabaka zao tofauti, wa karibu zaidi, kisha wa karibu kulingana ukaribu wao na mahitaji. Kwa hivyo, kuwapa matumizi ni sadaka na kuunga ukoo “na mayatima”. Nao ni watoto wadogo ambao hawana wa kuwachumia. Basi, wao kwa kawaida huwa wahitaji kwa sababu ya kutoweza kujisimamia masilahi ya nafsi zao, na kumpoteza anayewachumia. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawausia waja wake juu yao, kwa rehema yake na huruma yake juu yao. “Na masikini”. Nao ni watu wenye mahitaji ya lazima, na wenye mahitaji ya lazima ambao mahitaji yaliwanyamazisha. Basi wanapewa ili kuwatimizia mahitaji yao na kuwatosheleza. “Na msafiri” yani mgeni aliyekatikiwa katika nchi isiyokuwa yake. Basi atasaidiwa juu ya safari yake kwa matumizi ambayo yatamfikisha kwenye pahali anapokwenda. Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowachagua watu wa haya makundi kwa sababu ya ugumu wa mahitaji yao, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajumlisha, akasema: “Na chochote mnachofanya katika heri” kama vile sadaka mnayowapa hawa na wengineo, bali katika kila aina ya utiifu na ibada, kwa sababu zinaingia katika jina ‘heri.’ “Basi Mwenyezi Mungu kwa hakika anaijua.” Atawalipa juu yake, na atawahifadhia hayo, kila mmoja kulingana na nia yake na ikhlasi yake, na wingi wa kutoa kwake na uchache wake, na ukali wa haja yake juu yake, na ukubwa wa athari yake na manufaa yake.