انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢٨

لَقَدْ جَآءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِٱلْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ١٢٨

{128} Yeye Mtukufu anawakumbusha waja wake Waumini juu ya kuwatumia Nabii asiyejua kusoma na kuandika, ambaye ni kutokana na wao wenyewe, ambaye wanaijua hali yake, na wanaweza kujifunza kutoka kwake, na wala hawajizuii na jambo la kutomfuata, ilhali yeye Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - anawashauri sana na anafanya bidii katika masilahi yao. "Yanamhuzunisha yale yanayowataabisha;” yaani, ni gumu kwake jambo ambalo ni gumu kwenu linamtaabisha. "Anawajali sana” kwa hivyo anawapendea heri, na anafanya jitihada yake yote katika kuifikisha kwenu, ana anawania juu ya kuwaongoza kwenda katika imani, anachukia uovu juu yenu, na anafanya jitihada yake yote kuwaepusha nao. "Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma.” Yaani, yeye ni mwenye huruma mkubwa, anawahurumia kwa zaidi ya wazazi wao, na kwa sababu ya hili ndiyo ikawa haki yake inatangulizwa mbele ya haki zote za viumbe, na ni wajibu kwa umma kumwamini, na kumfanyia taadhima, na kumheshimu, na kumsaidia.