انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢٧

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتْ سُورَةٌ نَّظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَىٰكُم مِّنْ أَحَدٍ ثُمَّ ٱنصَرَفُوا۟ ۚ صَرَفَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ ١٢٧

Na kauli yake:

{127} Yaani, wanafiki wanaotahadhari kwamba kuteremshiwa Sura inayowaambia yale yaliyo katika nyoyo zao. Na sura inapotereka ili waiamini na watende kwa mujibu wa yaliyomo, "hutazamana wao kwa wao" huku wameazimia kuacha kuifanyia kazi, wanangojea fursa itokee wanapokuwa mbali na macho ya Waumini, na husema: "Je, yuko yeyote anayewaona nyinyi? Kisha huondoka wakaenda” kwa kukwepa, na wanakwenda hali ya kuwa wamepeana mgongo; basi Mwenyezi Mungu akawalipa adhabu sawa na matendo yao. Kwa hivyo, namna walivyoacha kufanya matendo mema, “Mwenyezi akaziondoa nyoyo zao.” Yaani akazizuia kufikia haki na akaachilia mbali, "kwa kuwa hao ni kaumu wasiofahamu.” Kufahamu kwenye kuwanufaisha. Kwani kama wangefahamu, basi wangekuwa inapoteremshwa Sura wanaiamini na kuifuata amri yake. Na kinachokusudiwa katika haya ni kubainisha ukubwa wa kujiweka mbali kwao na jihadi na mengineyo miongoni mwa sheria za imani; kama alivyosema Yeye Mtukufu kuwahusu, “Na inapoteremshwa Sura madhubuti na vikatajwa ndani yake vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa yule anayezimia kwa mauti.”