التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَا كَانَ ٱسْتِغْفَارُ إِبْرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَآ إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُۥٓ أَنَّهُۥ عَدُوٌّ لِّلَّهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَٰهِيمَ لَأَوَّٰهٌ حَلِيمٌ ١١٤
{114} Na hata kama kuomba msamaha kulipatikana kutoka kwa rafiki mwandani wa Mwingi wa Rehema, Ibrahim, amani iwe juu yake, juu ya baba yake, basi hilo ni kwa sababu ya “ahadi aliyomuahidi” na hilo ni kabla ya kujua mwisho wa baba yake. "Lakini ilipombainikia” Ibrahim kwamba baba yake “ni adui wa Mwenyezi Mungu," na atakufia katika ukafiri wake, na mawaidha na ukumbusho hayatamfaa kitu; "alijiweka mbali naye," kwa kuafikiana na Mola wake Mlezi na kumfanyia adabu nzuri. "Hakika Ibrahim alikuwa mwingi wa kuomba." Yaani, mwenye kurudi kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yote, mwingi wa kumtaja na kuomba dua, na kuomba msamaha, na kurejea kwa Mola wake Mlezi. "Mvumilivu;" yaani, mwenye kuwahurumia viumbe, na kusamehe makosa yao, hachukizwi na ujinga wa wajinga, wala hamkabili mwenye kumkosea kwa kosa lake. Baba yake alimwambia: "Mimi hakika nitakupiga mawe," na akamwambia: "Amani iwe juu yako, nitakuombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi." Basi ni lazima muige na mufuate mila ya Ibrahim katika kila jambo isipokuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: "Lazima nitawaombea msamaha;" kama Mwenyezi Mungu alivyowatanabahisha juu yake na mengineyo. Na ndiyo maana akasema: