التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
مَا كَانَ لِلنَّبِىِّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَن يَسْتَغْفِرُوا۟ لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوٓا۟ أُو۟لِى قُرْبَىٰ مِنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَحِيمِ ١١٣
{113} Yaani, haimfailii Nabii na Waumini wala sio vizuri kwao "kuwaombea msamaha washirikina.” Yaani, yule aliyemkufuru na akaabudu asiyekuwa yeye pamoja naye, "hata wakiwa ni jamaa zao, baada ya kwisha wabainikia kuwa hao ni watu wa Motoni.” Kwa maana kuwaombea msamaha katika hali hii ni kosa, na hakuna faida. Basi haiwafailii Nabii na Waumini kwamba wanapokufia katika ushirikina au ikajulikana kuwa watakufa wakiwa hivyo, basi neno la adhabu linakuwa limeshawajibika juu yao, na ikawajibika kwao kudumu katika Moto, na wala uombezi wa waombezi wala kuomba msamaha kwa wanaoomba msamaha hakutawafaa. Na pia, ni juu ya Nabii na wale walioamini pamoja naye waafikiane na Mola wao Mlezi katika radhi yake na ghadhabu yake, na wawe marafiki wa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfanya kuwa rafiki, na wawe adui kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfanya kuwa adui. Na kuwaombea kwao maghufira kwa yule aliyebainika kwamba yeye ni katika wenza wa Moto kunapingana na hilo na ni kinyume nalo.